Saturday, July 28, 2007

WASIFU WA ALI MWINYI MSUKO

CURICULUM VITAE

JINA KAMILI: Ali Mwinyi Msuko
TAREHE YA KUZALIWA: 01.01.1960
MAHALI PAKUZALIWA:
KIJIJI: Mitakawani
WILAYA: Kati
MKOA: Kusini Unguja

ELIMU
· MSINGI: 1966 – 1973 Skuli ya Uzini
· SEKONDARI YA AWALI: 1974 – 1976 Skuli ya Uzini
· CHETI CHA KIDATU CHA IV 1979 Privet
· CHETI CHA UALIMU DARJA III A: 1980 – 1982 Nkurumah
· STASHAHADA YA SAYANSI YA JAMII: 1985 – 1986 Higher Komsomol School Moscow USSR
· MAFUNZO YA SIASA NA ULINZI: 1976 Kambi ya Viana U/Ukuu
· MAFUNZO YA MAKADA WA KUSUKUMA MBELE MAPINDUZI YA KILIMO: 1988 Chuo cha CC M Zanzibar
· MFUNZO YA UALIMU WA VIJANA NA CIPUKIZI:
1979 Chuo cha Elimu ya Taifa Kleruu Iringa
· MAFUNZO YA MAKADA WA CCM CHO CHA CCM HURIA: 2004 – 2005
· MAFUNZO YA KAMATI ZA UTENDAJI ZA CCM WILAYA: 1998 Wete Pemba



KAZI NILIZOWAHI KUZIFANYA.
§ Mwalimu wa Shule za Msingi na Sekondari
§ Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Itikadi na Uenezi
§ Katibu wa UVCCM Wilaya
§ Katibu Msaidizi Mkuu Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar
§ Katibu wa UVCCM Mkoa
§ Katibu wa CCM wilaya

KAZI YA SASA
Katibu Msaidizi Idara ya Itikadi na Uenezi Afisi Kuu ya CCM Zanzibar

UZOEFU WA UONGOZI KATIKA CHAMA NA JUMUIYA
§ Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa ASP Tawi la Shule 1976
§ Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM WA Tawi 1978 – 1983
§ Katibu wa Chipukizi wa Wilaya 1979 – 1983
§ Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya I/Uenezi 1987 – 1992
§ Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya 1992 – 1996
§ Katibu Msaidizi Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM
Afisi Kuu Zanzibar 1996 – 1997
§ Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa 1997 – 1998
§ Katibu wa CCM Wilaya 1998 – 2001
§ Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji WAZAZI Wilaya 1984 – 1989
§ Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana
CCM Mkoa 1988 – 1993
§ Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana
wa CCM Taifa 1988 - 1993
§ Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa 1987 – 1992
§ Katibu wa CCM Tawi la Afisi Kuu Zanzibar 2002 – 2007
§ Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 1990
§ Mjumbe wa Kamati ya Usafiri Mapokezi na Malazi
§ ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa 2002, 2005na 2006
§ Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya H/Kuu ya Tawi la
§ Kijijini (Umbuji) 2007 – 2012
§ Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi la CCM Afisi Kuu
Zanzibar 2007 - 2012

Wednesday, July 18, 2007

JEMBE NA NYUNDO SIO MSALABA

JEMBE NA NYUNDO SIO MSALABA

WATANZANIA wa rika yangu yaani wale wote wenye umri wa miaka hamsini na kuendelea waliozaliwa kabla na baada ya kuingia Wakoloni katika nchi mbali mbali Barani Afrika ikiwemo Tanzania, walikuwa mashuhuda wa jinsi wakoloni hao walivyolivamia Bara letu hili na kuwatawala wazee wetu ikiwa ni pamoja na kuwakandamiza, kuwanyanyasa na kuwatesa wananchi wake bila sababu ya msingi. Wakoloni hao walikuja kadhaa za Bara la Ulaya ikiwemo Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi n.k. walimimika kwa wingi Barani Afrika na kugawana mapande ya ardhi ambayo ni Mali halali ya Waafrika na kuanza kuzikalia nchi hizo pamoja na kuwatawala wananchi wake kwa mabavu. Sina haja ya kuelezea kwa upana zaidi juu ya madhila waliyoyapata mababu na wazazi wetu kwa wakati huo, kwani yanaeleweka kwa kila mtu wa Bara hili.

Kuna sababu nyingi zilizochangia kufanyika kwa uvamizi huo. Miongoni mwa sababu hizo ni kwamba wavamizi hao (Wazungu) walijua kuwa Barani Afrika ndilo bara pekee lenye kumiliki mali ghafi nyingi za aina kwa aina ambazo ni pamba, katani, buni, pareto, korosho, mbata, karafuu, n.k. Kama wangezipata bidhaa hizo zingewasidia kwa kiasi kikubwa sio tu kuimarisha viwanda vyao bali pia zingewaletea mapato makubwa zaidi na hivyo kuweza kujitajirisha na kuwa mataifa makubwa kama yalivyo hivi sasa. Waalifanya hivyo kwa vile Waafrika wenyewe walikuwa bado wapo kizani hadi wakafikia mahali wakaliita bara la watu wakizani (bara jeusi). Haya yote yalikuja kutokana na idadi kubwa ya watu wake walikuwa hawahui kusoma na kuandika.

Wahenga walisema “kila penye mbaya wako na mwema wako yupo”. Pamoja na ukweli kuwa wakoloni walikuwa watu wabaya, lakini pia walikuwepo wengine wazuri. Wakijua kuwa watu wanaowatawala hawana elimu kabisa. Wale wenye mioyo mizuri walijaribu kuanzisha shule (skuli) katika badhi ya nchi barani humu na kuwapatia masomo angalau ya kujua kusoma na kuandika. Hali hiyo iliendelea kidogo kidogo hadi kufikia hapa tulipo na kwamba baadhi ya Waafrika waliweza kupata elimu nzuri kiasi cha kujivunia. Aidha, wakiwa na na hivyo kuweza kuelekeza nguvu zaidi katika mapambano dhidi ya wakoloni hao na kadri siku zilivyosonga mbele ndio mapambano yalizidi kupamba moto hadi kufikia Bara zima kuwa huru.

Mapambano ya kutafuta uhuru kwa kila nchi ya Bara la Afrika yalisimamiwa na baadhi ya wana haraka wa nchi husika. Mathalan, aliyeongoza mapambano ya kutafuta uhuru wa nchi iliyokuwa Tanganyika iliyokuwa chini ya Ukoloni wa Kijerumani ni Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Visiwa vya Zanzibar, vilivyotawaliwa na Ukoloni wa Kisultan wa Oman, alikuwa Hayati Mzee Abeid Amani Karume. Watu wengine mashuhuri waliosimama kidete kuhakikisha nchi zao zinakuwa huru ni Jomo Kenyatta (Kenya), Kwame Nkurumah (Ghana), Ahmed Ben Bella (Tunisia), Ahmed Sekouture (Guinea), William Tolbert (Liberia), Kenneth Kaunda (Zambia), Nelson Mandela (SA), n.k. Hao ni baadhi tu lakini kuna wengine kadhaa walioongoza mapambano hayo katika nchi zao hadi kufikia ukombozi kamili.

Mwalimu Julius K. Nyerere, chini ya Chama cha TANU, aliongoza mapambano ya kutafuta uhuru wa Tanganyika kwa muda wa miaka saba (7) – yaani 1954 hadi Disemba 09, 1961, ambapo Tanzanyika ilipopata uhuru. Kwa upande Zanzibar, Hayati Mzee Abeid Amani Karume, chini ya Chama cha Afro Shirazi (ASP), naye kwa muda wa miaka isiyopungua sita (6), aliongoza mapambano dhidi ya ukoloni wa kisultani kuanzia 1957 - Januari 12, 1964, Zanzibar ilipojikomboa katika madhila ya ukoloni na hivyo kuleta faraja kubwa kwa wananchi na hasa wazalendo wa Unguja na Pemba.

Kutokana na busara na hekima za Mzee Karume na Mwalimu Nyerere, kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar na Tanganyika, waliweza kuziunganisha nchi hizi mbili hapo Aprili 26, 1964 na kuifanya kuwa nchi moja iliyojulikana kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja na kuungana huko lakini Serikali ziliendelea kubaki mbili ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanai (SMT), iliyoongozwa na Mwalimu J. K. Nyerere na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), chini ya Uongozi wa Mzee Abeid Amani Karume. Aidha, baada ya tukio hilo kubwa la kihistoria, Mzee Abeid A. Karume, alikamata Wadhifa wa Makamo wa Rais wa SMT. Lengo kuu la Muungano huo linaeleweka na kila mmoja wetu nalo sio jengine bali ni kuimarisha zaidi masuala ya ulinzi wa ndani na nje ya mipaka yetu.

Tangu kuasisiwa kwa Muungano huo, Watanzania tumeshuhudia mambo mengi ya maendeleo yaliyosimamia kwa ujasiri na umahiri mkubwa wa viongozi wetu hao. Lakini kuwa na jambo moja la msingi la kujiuliza na kila Mtanzania ? Iweje nchi ya Muungano yenye Rais mmoja iwe na Vyama viwili tofauti ?.

Ilichukua muda wa miaka takriban kumi na mitatu (13), ambapo Watanzania waliposhuhudia Viongozi wao wa Vyama vya TANU na ASP – yaani Mwalimu Julius . K. Nyerere na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi (Awamu ya Pili), wakiamua kwa kauli moja na kuviunganisha Vyama hivyo na kuwa Chama Kimoja, Chama chenye nguvu na imara zaidi. Aidha, uunganishaji wa Vyama hivyo kungeweza kujibu suali lililojengeka na kutawala nafsi za Watanzania walio wengi kwamba itawazekanaje nchi yenye Rais mmoja iwe na vyama viwili vyenye itikadi moja ?.

Jibu la suali hili lilipatiwa ufumbuzi Februari 5, 1977, wakati Vyama vya TANU na ASP, vilipoungana na kufanya Chama Kimoja cha Siasa kilichojulikana kwa jina la CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM). Lakini kuzaliwa kwa CCM halikuwa ni tendo la kihistoria tu, bali pia kilikuwa ni kitendo cha kimapinduzi kwa vyama vya TANU na ASP, kukubali kujivunja vyenyewe kwa hiari, heshima na taadhima na kuunda Chama Kipya. Vilifanya hivyo ili kuweza kuendeleza harakati za Ukombozi wa Tanzania. Aidha, kitendo hicho ni uthibitisho tosha wa kukua na kukomaa kifikra, kinadharia, kivitendo na kimuundo kwa TANU na ASP. Kwa mantiki hiyo, wazo la kuunganisha vyama hivyo halikuwa jambo jipya kwa ASP na TANU. Mathalan, ASP ni matokeo ya Muungano baina ya ‘African Association’ na ‘Shirazi Association’.

Hivyo, kuzaliwa kwa CCM ni kitendo dhahiri cha kutekeleza Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1965 iliyosema “Kutakuwepo Chama Kimoja cha Siasa katika Tanzania …. Mpaka Vitakapoungana Chama cha TANU na ASP (ambavyo vikiungana vitaunda Chama Kimoja cha Siasa), lakini kwa sasa Chama cha Tanganyika kitakuwa TANU na Zanzibar kitakuwa Chama cha ASP”.

“Mwenye macho haambiwi tazama”. Kila Mtanzania amejionea mwenyewe jinsi CCM ilivyopania kuondoa kero mbali mbali zilizoikumba jamii ya Tanzania na kuleta maendeleo endelevu nchini humu kwa maslahi ya jamii nzima. Miongoni mwa mambo yaliyopatika ni pamoja na kuimarishwa kwa Mmiundombinu ya Kiuchumi na Ustawi wa Jamii, Mawasiliano, Afya, Elimu, n.k. Kama hiyo haitoshi, CCM imeweza kufanikisha azma yake ya kudumisha amani na utulivu wa Taifa letu.

Jambo la kushangaza na kwa kweli linasumbua kwa kiasi kikubwa nafsi za Watanzania walio wengi ni ile kauli ya kupotosha inayotolewa na kusambazwa na baadhi ya Watanzania kwamba “CCM SIO CHAMA CHA WANANCHI WA TANZANIA NA KWAMBA NEMBO YA JEMBE NA NYUNDO ILIYOMO KWENYE BENDERA YAKE NI ALAMA YA MSALABA”. Hakika, kauli hiyo na nyengine kama hizo ni za kupotosha.

Wednesday, July 11, 2007

WAPINZANI KUSHINWA KABLA YA UCHAGUZI

Wapinzani wameshindwa hata kabla ya uchaguzi

Wakati tunakaribia katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar imebainika wazi kwamba hofu imewakumba wapinzani na hasa Chama cha Wananchi (CUF) kiasi cha viongozi wao kuashiria kushindwa kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika.

Dalili za kushindwa zianza zamani, pengine kabla ya kuanza kamapeni. Hofu hiyo iliibuka mara ya baada ya Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume kutangazwa kugembea tena nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi m(CCM).

Kabla ya mchakato wa kumpata mgombea huyo, wapinzani walikuwa wakifanya vibweka vingi huku wakijigamba kuwa wataing’oa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 30, mwaka huu.

Matumaini makubwa waliyokuwa nayo CUF ya kuishinda CCM yalitokana na mawazo yaliyokuwepo kwamba kuna utofahamiana miongoni mwa viongozi wa CCM na hivyo kuweka tama ya fisi ya kutegemea kudongoka mkono wa binadamu.

Kimsingi, mawazo hayo yaliyobeba hisia za propaganda chafu yalikuwa na malengo ya kutaka kuwahadaa wafuasi wa CCM na kuwachanganya viongozi wao kabla ya kuanza mchakato wake wa kumpata nahodha atakayeipeperusha bendera yake katika kinyang’anyiro cha urais.

Katika kuiangalia propaganda hiyo, imebainika dhahiri kwamba ilitokana na woga, hofu na waswasi wa kuangushwa vibaya katika kinyang’anyiro hicho,
Baada ya wapinzani kutofanikiwa hila zao za kuingiza mamluki katika uandikishaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura.

Si hivyo tu, lakini CUF katika kujitafutia uhalali wa kuwa chama pekee chenye upinzani wenye nguvu Zanzibar, kilijaribu sana kutaka kuvizuia vyama vingine vya upinzani visiweke wagomea katika nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Mbinu hiyo ilikuwa ni kutaka kuhakikisha kwamba wafuasi wote wa upinzani wanampigia kura mgombea wa CUF katika nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar.

Hilo halikuwezekana kwani vyama vitano vimejitokeza kuweka wagombea wao. Vyama hivyo ni CCM, CUF, Jahazi asilia, UDP na

Kutokana na hali hiyo, inajitokeza wazi kwamba uchaguzi wa mwaka huu, mambo yatakuwa mambo kweli kwani takriban vyama vyote vilivyosimamisha wagombea wao vimeadhimia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo na sio kuibeba CUF ambayo hivi sasa inahitaji kupatiwa msaada wa damu kutoka kwa vyama hivyo.

DALILI ZA KUSHINDWA
Wakati wakujifaragua kwamba mwaka huu lazima CUF ipate ridhaa ya wananchi kuongoza dola, majinato yao yamekoma baada ya hila zao nyingi kushindwa.

Hila za CUF zilianza kukwama tokea wakati wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ulipoanza kisiwani Unguja. Kilichoandaliwa na chama hicho katika uandikishaji huo ni kupandikiza watu wasio na sifa za ukaazi.

Kwa kutumia wafuasi wa chama hicho wanaoishi katika mikoa ya Tanzania Bara, Kenya na nchi za Ghuba, CUF ilijipanga kuandiokisha wapiga kura wengi. Mbinu hiyo iligunduliwa na CCM kwa kutotoa mwanya wa kuandikishwa wasiohusika kwenye daftari hilo la wapiga kura.

Kushindwa kwa mbinu hiyo kuliishia kwa chama hicho kutoa malalamiko yaliyodai kutoandikishwa wafuasi wao wapatao 10,000. Malalamiko hayo yalikuwa ni kuashiria kukubali kushindwa.

Kwa kufahamu kwamba idadi ya walioandikishwa kwenye daftari la wapiga kura haiwezi kukipatia CUF ushindi katika Uchaguzi Mkuu, hila ya kutaka kulichafua daftari hilo zilionekana kushamiri. Kwa kuitumia kampuni ya Waymark kulijitokeza ishara za wazi za kiharamia zilizofanya na kampuni hiyo.

Miongoni mwa uharamia uliofanywa na kampuni hiyo ni kuibwa majina ya wapiga kura 30,000 baada ya kampuni hiyo kuruhusiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuhakiki kwa majaribio majina ya wapiga kura 10,000.

Aidha, mipango ilikuwa inafanywa na kulisafirisha nje ya nchi daftari la wapiga kura kwa kisingizio cha kwenda kulihakiki ili kubaini majina ya wapiga kura wanaofaa na wasiofaa. Kitendo hicho kilikuwa ni cha kutiliwa mashaka makubwa hasa baada ya kubainika wizi uliokwishafanyika wa majina 30,000 ya wapiga kura.

CCM ilitegua mtego huo uliowekwa ambao ulikuwa na mkakati maalumu wa kuharibu daftari hiyo kwa maslahi ya kuwapendelea wapinzani. Kugunduliwa kwa mtego huo pia kulipelekea CUF kulalamika kiasi cha kutishia kugomea kushiriki kwenye uchaguzi wenyewe iwapo hakukufanyika uhakiki. Malalamiko hayo pia yanaashiria kukubali kushindwa.

Kipigo walichokipata wapinzani kilichotokana na utambulisho wa kishindo ulioambatana na umati wa wananchi waliojitokeza kumuunga mkono mgombea huyo wa CCM, Abeid Amani Karume alipokwenda Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu za kugombea Urais kilitosha kubainisha kukubalika kwake kwa umma.

Umati huo wa watu ulitoa taswira kamili ya CUF kushindwa kwani pamoja na wapinzani kwa muda mrefu kujilabu kwamba wanaungwa mkono na wananchi wengi, siku hiyo ilionekana wazi kuwa mawazo hayo yaliyokuwa ni kinyume chake.

Katika harakati za kutambulishwa wagombea wa CCM baada ya kuteuliwa na chama chao viongozi wa kitaifa wa CUF walikuwa wa kwanza kutangaza kulalamikia utambulisho huo. Madai waliyoyatoa ni kuwa CCM imeanza kampeni kabla ya wakati huku viongozi hao wa upinzani wakisahau mikutano waliyokuwa wakiifanya katika kuwahamasisha wafuasi wao kujiandaa mithili ya wanasuburi kwenda vitani.

Viongozi hao wa CUF pamoja na kulalamika kuwa CCM imeanza kampeni kabla ya wakati, walikuwa wakitishwa na wimbi la wafuasi wake wakiwemo viongozi waandamizi na Wabunge wa chama hicho kujitoa na kujiunga na CCM. Matukio hayo ni dalili tosha zinazoashiria kushindwa kwa chama hicho.




Mbali na hali hiyo CUF, tayari imeshalalamika kuwa uchaguzi huenda usiwe huru na wa haki kwa sababu ya kutokuwa na imani na mchakato mzima wa kuandikisha wapiga kura.

Tamko la Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad la kubainisha kwamba hatokubali mmatokeo yoyote ya uchaguzi hata endapo yeye mwenyewe atashinda lilitosha kubainisha kulia uteka. Matamshi hayo ni sehemu ya kukata tama kabla ya hata uchaguzi haujafanyika.

Vigezo vyote hivyo vinaweka bayana kushindwa kwa CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utakaofanyika Oktoba 30, 2005. Hali hiyo sasa inafahamika hata kwa baadhi ya wafuasi wa chama hicho na ndiyo iliyoshusha hamasa za wafuasi hao za kwenda kwa wingi katika mikutano ya hadhara imepungua sana hivi sasa ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla.

CUF iliyozoea kushindwa na badala yake kudai kuwa wameibiwa kura kama ilivyofanya mwaka 1995 na 2000, tayari imeshaonesha dalili za kushindwa tena mara ya tatu mfululizo ambapo viongozi wa chama hicho wanaeleza wazo kuwa kuwa huenda mambo yakawa kama yalivyokuwa chaguzi ziliopita.

Kwa kufahamu hivyo, ndio maana chama hicho kikatoa tamko la kutaka kususia uchaguzi Zanizbar iwapo madai kilichotoa juu ya hitilafu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hazitapatiwa ufumbuzi kwa muda maalumu uliotolewa ambao umeshamalizika.

Kinachodhihirika ni kubainika wazi kwamba upinzani umeshashindwa hata kabla ya kupigwa kura. Na kinachoshindilia msumari wa mwisho katika jeneza hilo la CUF ni kujitokeza kwa wingi wafuasi wa CCM kwenye mikutano ya kampeni ya CCM. Wingi huo unaifanya CCM kuendelea kuzoa kura katika uchaguzi ujao na dalili tosha ya ushindi wa kishindo.

VOTI KWA CCM

VOTI KWA CCM


Kwanza kabisa sina budi kumshukuru Mwenye Munngu Mtukufu kwa kutujaalia uzima na afya njema na pia kutupa uwezo wa kutekeleza sunna muhimu ya Funga iliyokokotezwa na Mola Karima ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan, kwa wale Waumini wa Dini ya Kiislam.

Ndugu wana CCM na wananchi kwa ujumla, kama mjuavyo, kesho ni siku ya Jumapili tarehe 30 Oktoba, 2005. Ni siku muhimu sana katika historia ya Taifa letu la Tanzania Zanzibar. Ni siku iliyopangwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu, kwa lengo la kuwachagua viongozi mbali mbali wa kitaifa ikiwa ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.

Chama cha Mapinduzi kinaamini kwamba wananchi walio wengi wa Unguja na Pemba, wanauelewa mkubwa hususan masula ya kisiasa na kwamba watakuwa tayari kuitumia kikamilifu haki zao za kikatiba na kidemokrasia, jambo ambalo linatoa faraja kubwa sana kwa CCM. Kwa kuzingatia hali hiyo, sina budi kuwanasihi wana CCM na wananchi wapenda amani na utulivu wote kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kwenda vituoni Mijini na Vijijini kwa dhamira moja tu nayo sio nyengine bali kwa ajili ya kupiga kura. Kufanya hivyo mtakuwa tayari mmetekeleza vyema haki yenu hiyo ya kuchagua viongozi mnaowataka katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2005.

Chama cha Mapinduzi kinawataka kuwatoa wasiwasi wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba kuwa kuna njama na hila zilizopangwa na baadhi ya vyama vya upinzani vyenye lengo la kutaka sio tu kuwatisha wananchi na hasa wana CCM ili washindwe kwenda vituoni kupiga kura zao bali pia wanakusudia kuvuruga Uchaguzi huo na hivyo usifanyika kama ilivyokusudiwa.

Kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi nachukua fursa hii kuwahakikishia wana CCM na wananchi wapenda amani wote wa Taifa hili kwamba ulinzi umeimarishwa mara dufu na hivyo hakuna mtu au kikundi cha watu kitakachopata nafasi ya kutisha watu mitaani katika siku hiyo tu ya upigaji kura bali hata baada ya shughuli hiyo nzito kukamilika. Kikubwa zaidi ni kujitokeza mapema katika vituo mlivyopangiwa na kufanya shughuli hiyo muhimu na kuwachagua viongozi mnaowataka na hasa wagombea wote wa CCM ili waweze kuendelea kuwaleta maendeleo endelevu kwa maslahi yenu na vizazi vyenu vya leo na vijavyo bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Kwa kuwa haki ya kupiga kura ni ya kila raia aliyetimiza umri na masharti yaliyowekwa na Tume ya Uchaguzi, Chama chetu cha Mapinduzi, kitaendelea na juhudi zake ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyombo vya dola kuimarisha zaidi ulinzi ili kila raia na hasa kila mzalendo mwenye haki ya kupiga kura aweze kuitumia vyema haki yake hiyo. Hivyo, ndugu wana CCM na wananchi msikubali kubabaishwa kwa kauli za uzushi zinazotolewa na watu mitaani kwani hali ya ulinzi imeimarishwa kwa kiwango cha hali ya juu mno. Jambo la msingi ni kuamka asubuhi mapema, nenda kituoni, jipange kwenye mstari, piga kura yako kwa kuwachagua wagombea wote wa CCM kuanzia Mgombea wa Kiti cha Urais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani. Ukimaliza kufanya hivyo rejea nyumbani kusubiri matokeo yatakapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hatimaye ushangilie ushindi.

Kwa nini tunasema hivyo? Tunasema hivyo kwa sababu Chama cha Mapinduzi ndio Chama pekee chenye wanachama na wapenzi wengi zaidi kuliko Chama chengine chochote cha siasa hapa nchini. Aidha ni Chama pekee chenye nia thabiti ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kutokana na Sera zake zinazotekelezeka siku hadi siku. Sote ni mashuhuda wa jinsi gani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume, alivyofanikiwa kusambaza kwa kiwango cha hali ya juu mno ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2000. Sina haja ya kuyataja yote yaliyopatikana. Miongoni mwake ni pamoja na :-

· Uchumi wa Taifa umekua kwa asilimia sita nukta tano (6.5%) pamoja na kusimamia vyema matumizi ya mapato.
· Miundo mbinu
Barabara mpya kwa kiwango cha lami zimejengwa Unguja na Pemba.
· Vituo vya Afya vimejengwa Mijini na Vijijini
· Umeme – umesambazwa karibu nchi nzima
· Maji safi na salama yanapatikana Mijini na Vijijini
· Serikali imefanikiwa kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji
· Sekta ya Elimu
i) Skuli zimeenea na mabanda yameongezeka mara dufu
ii) Vyuo Vikuu hadi kufikia vitatu
· Mawasiliano na Uchukuzi
i) Makampuni ya Simu za mkononi kama vile Zantel, Vodacom, Mobitel, Celtel n.k. zimeanzishwa na kuendelea vizuri.
ii) Usafiri wa Anga na baharini vimeimarishwa
iii) Viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba vimepanuliwa n.k.

Kwa mantiki hiyo, wapinzani hawana uwezo wa kuishinda CCM katika Uchaguzi Mkuu huu, kwa sababu hawana Demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyao. Hivyo, natumia fursa hii kuwaomba wana CCM na wananchi wapenda amani wote kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kwa salama na amani. Baada ya kukamilisha kupiga kura yako, ondoka na urejee nyumbani bila ya tatizo lolote. Aidha, Chama cha Mapinduzi kinawaomba wana CCM wote kutovaa sare za Chama chetu. Hili sio ombi bali ni amri, kwani kuvaa sare kwa siku ya kupiga kura ni kosa la jinai.

UJIO WA WAANGALIZI WA KITAIFA NA KIMATAIFA:
Chama cha Mapinduzi kimefarajika na hali ya ujio wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Madola waliofika nchini kwa lengo la kuja kuangalia jinsi Uchaguzi huu utakavyofanyika. Aidha, nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa kumiminika kwa wingi. Lakini CCM inasema kwa kuja nchini humu kwa lengo la kuja kushuhudia jinsi gani Uchaguzi unavyofanyika na sio wamekuja kutoa maelekezo ya jinsi gani Uchaguzi huu ufanyike wala kutoa matokeo ya Uchaguzi huo.

Chama Cha Mapinduzi kinaamini kuwa kuwepo kwao kutasaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha taarifa sahihi kwenye Jumuiya ya Kimataifa kuhusiana na hali halisi ilivyo kuanzia uwingi wa wanachama na hata wapenzi na pia jinsi gani walivyohamasika na kuwa tayari wakisubiri siku yenyewe kufika ili waweze kutumia haki zao za kidemokrasia na kuchagua viongozi wanaowataka bila ya wasiwasi wowote. Aidha, kuwepo kwao kutasaidia kubainisha ukweli na uongo wa viongozi wa vyama vya upinzani wanaojaribu kuihadaa dunia eti CCM haina wanachama na pia hawapendwi na jamii ya Wazanzibari. Kupitia mkutano wa Ufungaji wa Kampeni za CCM uliofanyika leo, tunaimani kubwa kwamba Waangalizi wameweza kujionea wenyewe hali halisi na hivyo kuweza kupima na kutambua ukweli na uongo wa vyama hivyo vya upinzani nchini.

Mwisho, kwa mara nyengine tena nachukua fursa hii kuwataka wana CCM na wananchi wapenda amani na utulivu wote wa Taifa letu, kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura ili kwenda kupiga kura zenu na kukipatia ushindi wa nguvu ya tsunami Chama chenu cha Mapinduzi na hivyo kukipa ridhaa kwa mara nyengine tena ya kuongoza dola kwa miaka mingine mitano ijayo.

Ahsanteni.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.


(VUAI ALI VUAI)
KATIBU – IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
ZANZIBAR.

Monday, July 9, 2007

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama na wafuasi wake kutobabaika na kauli zilizotolewa na CUF za kudai kwamba kuna vijana wengi wa CCM wamejiunga na chama hicho cha upinzani.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Bwana Vuai Ali Vuai, +imeeleza kuwa kauli hizo ni za uongo na hakuna mwanachama yeyote aliyehama CCM na kujiunga CUF.

Bwana Vuai ameeleza kuwa baada ya kufuatilia kauli hiyo katika maeneo yaliyoelezwa kwamba kuna vijana waliojiunga na chama hicho, CCM imebaini kuwa taarifa hizo zilikuwa hazina ukweli.

Ameeleza kwamba kutokana na kufuatilia huko imefahamika vijana waliotangazwa kutoka CCM ni miongoni mwa vijana wa chama hicho cha upinzani wa maeneo ya Shangani huko Mkokotoni ambao walipangwa kurejesha kadi za kughushi ambazo hazikuwa kadi halali za CCM.

Amewataka wananchi kutobabaishwa na propaganda za uongo ambazo ni mfululizo wa kauli za upotoshwaji zinazotolewa na viongozi wa CUF kwa vipindi chote hata kabla ya kuanza kwa mikutano ya kampeni.

Bwana Vuai alisema viongozi wa upinzani wamekuwa wakifanya hivyo kwa kufahamu kwamba CCM itaendelea kushinda katika uchaguzi ujao Tanzania Bara na Zanzibar kutokana na kukubalika kwake mbele ya jamii.

Alifahamisha kuwa ushahidi wa CCM kuendelea kuongoza nchi unabainika kutokana na chama hicho kushinda viti 200 kabla ya hata uchaguzi vikiwemo viti vinane (8) vya ubunge na 192 udiwani.

Alieleza kuwa hicho ni kigezo tosha cha kuthibitisha kwamba wananchi wameridhika na utekelezaji wa ilani za CCM za mwaka 2000 ilisababisha kuimarika kwa miundo mbinu ya kiuchumi na ustawi wa jamii nchini.

Hivyo, Bwana Vuai ameitaka CUF kuacha mara moja kutoa kauli za kubabaisha kwani kufanya hivyo ni kuzidi kuidhihirishia dunia kuwa tayari kimekata tamaa ya kupata ushindi kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 30, mwaka huu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


………………
(Vuai Ali Vuai)
Katibu – Idara ya Itikadi na Uenezi
Chama cha Mapinduzi
ZANZIBAR

20/10/2005
Ndugu Mhariri

Naomba nafasi ili niweze kutoa maoni yangu juu ya bei ya mafuta iliyopo hapa nchini.

Ni muda mrefu sasa tokea Bodi ya Mapato nchini kupitia Afisa wake wa kodi kututangazia Wazanzibari kuwa Serikali imejitoa katika kudhibiti bei za mafuta nchini ili wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wapange bei kwa mujibu wa gharama halisi za biashara hiyo.

Kutokana na ufahamu wangu mdogo wa biashara nilitegemea kuwa bei ya mafuta nchini hivi sasa ingepungua kama ilivyo nchi nyingi duniani kutokana nakuongezeka uzalishaji hasa nchi zenye kuzalisha kwa wingi mafuta (OPEC). Vile vile, kwa upande wa shilingi ya Tanzania nayo imeimarika kidogo siku hizi thamani yake kuliko kipindi ambacho bei ya mafuta ilipanda hadi kufikia bei Tshs. 1350, kwa Petroli na 1320 kwa Disel. Kipindi hicho dola moja ya Kimarekani ilikuwa niTshs. 1320 kuinunua. Hivi sasa dola moja ya Kimarekani ni Tshs. 1275 kuinunua. Wakati huo huo, Pipa moja la mafuta hapo kabla katika Soko la Kimataifa likiuzwa dola 79 na hivi sasa ni dola 62.

Kwa hiyo,kutokana na mwenendo huo wa bei, kimataifa ilitakiwa bei ya mafuta nchini nayo ipungue hasa kutokana na Serikali kujitoa katika kuhodhi bei ya mafuta nchini na kwa uchache bei iwe kama ilivyo Tanzania Bara ambapo bei hivi sasa kwa lita moja ya Petroli haizidi 1270 hata kwa Mikoa iliyoko mbali na Bandari ya Dar es salaam.

Mwisho ningeiomba Wizara au Idara inayoshughulikia mwenendo mzima wa bei za bidhaa na huduma nchini kufuatilia kwa karibu zaidi bei zinazopangwa na wafanya biashara ambao hawajali maisha ya wananchi wa kawaida bali wanajali faida yao ili mpango wa kupunguza umasikini ufanikiwe nchini kwani kupanda kwa bei holela kwa bidhaa muhimu au kutopungua bei zake hata kama masoko mengine yamepunguza bei zake ni kutomtendea haki raia wa kawaida anaebebeshwa mzigo huo kwa njia isiyo ya moja kwa moja na maana halisi ya kuwepo soko huria itakuwa haina maana. Ni tegemeo langu kwamba Serikali nayo itaingilia kati suala hili pale inapoona kuna wakorofi wachache wanaoweka tamaa mbele kibiashara kuliko urahisia wake.


‘MWANANCHI MPENDA MAENDELEO’


………….
ALI SAID MUSSA
MAGOMENI
ZANZIBAR

JKAMPENI ZA UCHAGUZI MWEZI WA RAMADHANI

Ndugu Mhariri,

Napenda kuomba nafasi kupitia gazeti lako kutoa maoni yangu kuhusiana na mwenendo wa Uchaguzi unaoenedelea hivi sasa nchini tukiwa kwenye kipindi cha Kampeni.

Kwanza sina budi kutoa pongezi zangu kwa Chama Cha Mapinduzi kwa utaratibu wake wa kufanya mikutano ya Kampeni wakati wa asubuhi ili wanachama wake wapate nafasi ya kujitafutia riziki na kufanya Ibada katika kipindi hichi cha Ramadhani sote ni welewa wa mambo kuwa fadhila za mwezi wa Ramadhani kwa wanaofanya Ibada ni kubwa sana kuliko miezi mengine yoyote ya Kiislamu. Aidha Waisalamu wanatakiwa wawe waaminifu, wakweli na waungwana na kuepukana na kauli ambazo zitawafanya wasitafautiane na wale wasiofunga katika kipindi hichi. Vile vile yale yaliyomo kwenye dhamira zao yafuatane na vitendo vyao.

Nimeamua kutumia neno dhamira kwa kuwa ndio inayomuhukumu mtu hata kama jambo hajalifanya ila anakusudia kulifanya kwani tunaambiwa kwenye hadithi za Mtume kuwa “Hakika vitendo vinafuatana na nia na kila mtu atalipwa kutokana na nia yake” Kutokana na kukaribia Uchaguzi Mkuu na huku baadhi ya vyama tayari vishakata tamaa ya ushindi licha ya kutamka kuwa vitashinda hadharani ili kuwapa moyo wafuasi wake na kuwalaghai kwa ajili ya lengo lao waliloliweka na hasa baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 30/10/2005. Nimeamua kusema kuwa baadhi ya vyama vya Siasa vimekata tama ni kutokana na ushahidi nilionao wa watu hao kutumia mikutano ya siri na kututaka tujitayarishe kwa maandamano makubwa baada ya Uchaguzi ya kudai kupokonywa ushindi kinachonishangaza na kinachonifanya kuamua kuandika barua hii ni kutaka kuwatahadharisha wananchi wenzangu kuwa suala la kunyanganywa ushindi kwa atakaeshinda halitowezekana hata kidogo kutokana na taratibu nzuri zilizoandaliwa za kuhesabu kura na kutangaza matokeo kwa jumla ambapo vyama vyote vinatakiwa kuweka Mawakala bila ya shaka sote ni mashuhuda wa kauli za viongozi wakuu wote wa Vyama na hasa Chama Cha CUF ambao wamekiri wenyewe kuwa utaratibu ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi utapelekea kufanyika kwa Uchaguzi huru na wa haki. Sasa kinachonishangaza na kunifanya nikumbuke swaltul-Munafiqina ambayo imewaeleza kwa urefu na mapana watu ambao dhamira zao siku zote haziendeda na kauli zao ni kutaka kujua hayo maandamano wanayotaka kufanya ni kwa ajili ya nini na maslahi ya nani ikiwa tayari tumejenga uaminifu kwa Tume na tumekubali kuyapokea matokeo ya kura na haya ya Urais. Hivi viongozi wa CUF wanapotutaka siku watakayotutangazia kwa siri maandamano waliyoyatayarisha na kututaka tushiriki na kuwatanguliza wazee mbele kwa kile wanachokidai kuwa wakifa wao si hasara kwa kuwa washaonja chumvi nyingi na baadae wafuatie vijana na mwisho wanawake. Hivi ni kweli hawa viongzoi wa CUF wanaitakiwa mema nchi yetu na sisi wananchi?.

Jambo ninalotaka kuwaambia viongozi wa CUF ni kuwa wananchi wengi hivi sasa si wajinga na wanathamini uhai wao na wanafahamu kuwa mfa maji hukamata maji, kwa hiyo wasiwe na tamaa ya kutufanya chambo kwa kuwa tu bwana mmoja kakosa Urais. Hayo maandamano yake atakayoyafanya atayafanya yeye na Bwana Said wake ambao wamekula kiapo cha kufa kwa ajili yake na wale waliokata tamaa ya maisha lakini wengi tumechoka na ule wimbo wetu wa akikosa Seif tumekosa sote. Tukumbuke kuwa kupata au kukosa yote ni Majaaliwa. Na Mola amesema kuwa humpa Ufalme amtakae na humnyima amtakae. Hivi Maalim Seif akikosa yeye ndio atake sisi atufanye kuku wa muhanga? Kwa hilo tunamwambia hawai na tunamtakia kila la kheri katika maandamano atakayoyaongoza na kuzungukwa na hao wakubwa wake. Mwisho nawataka viongozi wa CUF wasome Shishtul Munafinna na hasa aya ya nane ya sura hiyo mwisho kabisa nawataka wana CUF wajue kuwa akishindwa Seif safari hii tisichoke kwani 2010 haiko mbali panapo uhai tumpe tena nafasi kwani kuvunjika kwa koko sio mwisho wa utunzi. La muhimu kwetu ni “AMANI” kwani hiyo ndio siri ya mafanikio na maendeleo na sio “UPANGA” utakaotupeleka kwenye hilaki. Mola tunakuomba utudumishie AMANI yetu dhidi ya Mahasidi wa nchi yetu. AMIN


RAIA MWEMA
ZANZIBAR

JIWE MOJA KWA NDEGE WAWILI

SHEREHE ZA KUTIMIA MIAKA 29 YA KUZALIWA KWA CCM NA USHINDI WA CCM KUTIMIA MWAKA MMOJA
“Tunasherehekea Chama chetu cha Mapinduzi Kuuwa Ndege Wawili kwa Jiwe moja….. Kwanza siku ya leo Februari 5 ya mwaka huu, Watanzania na hasa wana CCM tunasherehekea Chama chetu kimetimiza umri wa miaka 29 tangu kuzaliwa kwake hapo Februari 5, 1977. Pili Sherehe hizi zinakwenda sambamba na sherehe za ushindi mkubwa wa CCM kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Hayo ni baadhi tu ya maneno yaliyotamkwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zabnzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume, wakati akihutubia wana CCM na wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja katika mkutano wa hadhara wa kilele cha maadhimisho ya miaka 29 ya CCM – Februari 5, mwaka huu, uliofanyika Pwani Mchhangani, Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume. Mwandishi wa Makala haya ALI ABDULRAHMAN NDOTA, aliyefuatilia kwa karibu sherehe hizo anaelezea zaidi……

KILA ifikapo Februari 5 ya kila mwaka , wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Watanzania kwa ujumla, huwa wanasherehekea maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa kwa Chama chao. Mbali ya kawaida ya miaka iliyopita, wanachama hao wamesherehekea maadhimisho ya mwaka huu kwa staili ya aina yake, kwani wameshuhudia Chama chao kikitimiza umri wa miaka 29 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977.

Hakika, miaka 29 ni muda mfupi sana kuweza kupima maendeleo ya jamii. Hata hivyo muda huo unatosha kabisa kupima shughuli za Chama cha Siasa kinachoongoza nchi kama CCM na mafanikio yake. Sina haja ya kuelezea maendeleo yaliyoletwa hapa nchini na Serikali za Chama Cha Mapinduzi, kwani yanafahamika na kueleweka na kila mwananchi wa Taifa hili. Lakini nitakuwa mwingi wa fadhila endapo sitagusia kitu kwa upande wa maendeleo yaliyosambazwa na yanayoendelea kusambazwa siku hadi siku anchini humu.

Tangu Chama cha Mapinduzi kizaliwe miaka takriban ishirini na tisa iliyopita, Watanzania wenye umri huo na wale wa zaidi ya umri huo, wamekuwa mashuhuda wa jinsi CCM ilivyopania kuleta maendeleo endelevu kwa maslahi ya wananchi wake. Kila uchao, Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, zimekuwa mstari wa mbele katika kuwaondelea kero mbali mbali zinazowagusa wananchi wa Mijiji na Vijijini.

Katika kipindi cha hivi karibuni, kumejitokeza watu au kikundi cha watu kinachojaribu kutoa kauli za kejeli eti Serikali za CCM zimefanya nini cha kimaendeleo katika kipindi chote hicho cha miaka 29. Ama kweli “mwenye macho haambiwi tazama”. Mathalan, Serikali zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Searikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimefanikiwa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundo mbinu ya kiuchumi na ustawi wa jamii Mijijini na Vijijini. Lakini kubwa zaidi Serikali zote mbili za SMT na SMZ zimeweza kukusanya mapato kutoka vyanzio mbali mbali kwa kiasi kikubwa na pia zimefaulu kudhibiti matumizi mabaya (holela) ya mapato hayo. Aidha, zimefaulu kupunguza kama si kuziba kabisa mianya kadhaa iliyokuwa imeshamiri miongoni mwa wafanyakazi hasa wa shughuli za fedha nchini kote.

Hali hiyo imefikiwa baada ya Serikali hizo kuweka mikakati madhubuti ya kumiliki uchumi wa Tanzania usitumike kiholela ili kuwanyima nafasi wale wajanja wachache waliokuwa wakinufaika na mianya hiyo. Aidha, ongezeko hilo la mapato yanayokusanywa kwa kila mwezi, yameziwezesha Serikali za CCM kuweza kutoa ruzuku kwa vyama mbali mbali vya siaisa nchini ikiwemo Chama Tawala chenyewe (CCM).

Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya wafuasi au viongozi wa vyama vya upinzani wakitoa kauli za udanyanyifu zenye lengo la kupotosha jamii kwa kusema “eti CCM inafuja mapesa mengi ya wavuja-jasho wa Taifa hili kwa kufanya sherehe zisizokuwa na mpango wowote”. Jibu la hoja hiyo ni kwamba Chama cha Mapinduzi kamwe hakitumii na wala hakitotumia fedha za Serikali zinazotokana na wavuja jasho katika kufanikisha mipango yake ya kimaendeleo na shughuli nyengine za kawaida. Fedha zinazotumika ni sehemu ya ruzuku yake ya kila mwezi inayopatikana kutoka Serikalini kama wanavyopata vyama vyengine vya siasa nchini.

Ni ukweli usio shaka kwamba Chama cha Mapinduzi kilianza rasmi sherehe za maadhimisho ya miaka 29 Januari 30 na kufikia kilele chake Februari 05, mwaka huu. Wana CCM walisherehekea maadhimisho hayo yaliyofanyika Ki-Mikoa kwa kufanya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya mashindano ya michezo ya kijadi, resi za ngalawa na baiskeli pamoja na Tamasha la Muziki - lililorindima katika Kumbi mbali mbali za Starehe Mijini na Vijijini. Hakika ufanisi wa mambo hayo yote hauwezi kupatikana bila ya kuwepo fedha za kutosha. Hivyo, ukweli wa mambo unabaki pale pale kwamba fedha zilizotumika zinatokana na ruzuku itokayo Serikalini mwezi hadi mwezi.

Katika maadhimisho hayo, Chama cha Mapinduzi kimeweza kuwaalika viongzi wa vyama vyote vya siasa nchini ili kushiriki kikamilifu kwa maadhimisho hayo. Kwa bahati nzuri, ni viongozi wa vyama viwili tu ndio waliohudhuria kwenye sherehe hizo ikiwemo na mkutano wa hadhara wa mikoa mitatu ya Unguja. Viongozi wa vyama vya NLD na DP, ndio pekee walioshiriki katika sherehe za miaka 29 ya kuzaliwa kwa CCM iliyokwenda sambasamba na sherehe za ushindi mkubwa mithili ya tsunami katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka uliopita. Chama cha Mapinduzi kinatoa mkono wa pongezi kwa vyama hivyo na kwamba ndio vyama vinavyojua umuhimu wa kuwepo kwa demokrasia ya vyama vingi nchini. Chama cha Mapinduzi ni Chama pekee kilichokomaa kisiasa, kitaendelea na juhudi ya kuvilea vyama hivyo vikiongozwa na CUF hadi pale vitakapoweza kujisaidia na kujua lipi zuri na baya kwa maslahi ya jamii nzima ya Watanzania.

CCM imeshinda kwa ushindi wa tsunami katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, lakini wafuasi wa CUF wakiongozwa na viongozi wao, wamekuwa mstari wa mbele kukejeli ushindi huo siku hadi siku. Ati ushindi huo umetokana na wizi wa kiini macho…. Mara ushindi huo unatokana na vibwengo…. Na madai mengine chungu nzima. Kama hiyo haitoshi, wafuasi hao (CUF) wameanzisha mtindo wa kupandisha bei ya vyakula pamoja na baidhaa nyengine muhimu madukani ikiwemo nguo, huku wakiitumia falsa ya CCM ya “Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” kama shahada inayowaruhusu wao kupandisha kiholela bei za bidhaa hizo.

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume, akiwahutubia mamia ya wana CCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 29 ya CCM huko Pwani Mchangani, aliliweka bayana suala hilo na kusema kwamba “wale wote wanaotumia falsa hiyo kwa kwenda kinyume na maana yake waache mara moja kufanya upuuzi huo”. Alidai Rais Karume.

MAAMBUKIZI YA UKIMWI WA KISIASA

MAAMBUKIZI YA UKIMWI WA KISIASA

Ndugu Mhariri,

NAOMBA nami nikiwa mmoja kati ya wanajamii wa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nishiriki katika kutoa maoni yangu kuhusiana na tukio la aina yake lilotokea katika medani za kisiasa za Nchi yetu hivi karibuni ambapo Vyama vya Siasa vya kambi ya Upinzani vimesaini Mkataba wa Makubaliano (Memorundum of Understanding) ya kushirikiana katika kupambana dhidi ya Chama Tawala cha CCM.

Vyama vinne vya CUF, CHADEMA, TLP na NCCR – MAGEUZI vikiongozwa na Wenyeviti wao vilikutana katika Ofisi za Makao Mkuu ya Chama cha CUF na kukatibiana kwamba kuanzia sasa vitashirikiana bega kwa began a ikiwezekana zaidi ya hapo katika kuendesha shughuli zao za kisiasa katika kupambana na CCM na Serikali zake na kwamba katika Uchaguzi Mkuu ujao – wa mwaka 2010 vitasimamisha Mgombea mmoja wa Urais na kutozozana katika Majimbo ya Ubunge na Uwakilishi na hatimaye Udiwani na Uenyekiti wa Mitaa na Vitongoji. Vyombo vya Habari vilivyoripoti taarifa hizi waliyapa makubaliano haya majina tofauti wengine walikiita Ndoa, Ushirika na kadhalika.

Mimi kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza sana viongozi hawa na Vyama vyao kwa kuthubutu kutoka hadharani na kutwambia kwamba wao sasa ni wamoja ingawa Vyama ni tofauti. Lakini niwapongeze zaidi kwa nia waliyokuwa nayo kwamba safai haitoishia hapo, bali ni kuungana kabisa na kuwa Chama kimoja na kupunguza Utitiri wa Vyama katika Kambi ya Upinzani. Sasa tunasubiri kutekelezwa kwa nia yao hiyo njema.

Sasa naomba niweke bayana wasi wasi wangu niliyonao katika ndoa hii. Wanaharakati wa masuala ya jamii siku za hivi kaaribuni wamekuwa mstari wa mbele kabisa kusisitiza umuhimu wa kupima virusi vya UKIMWI kabla ya wanandoa wataarajiwa kufikia uamuzi wa kufunga ndoa zao. Binafsi yangu mimi naungana na wanaharakati hawa sio kwa jengine lolote bali kupunguza kasi ya maambukizi hivi vya Ukimwi (VVU) na hatimaye ndipo tutakapo tokomeza maaradhi hayo dhalili ya Ukimwi.

Sasa najiuliza jee ndoa hii ya wanandoa hawa wanne imepitia utaratibu huu tunaoelekezwa na wanaharakati hawa au ni ndoa ya Mkeka isiyoweza kusubiri achilia mbali kupimwa Ukimwi hata utaratibu mwanana wa ‘posa’ na ulipaji wa ‘mahari’.

Nimejiuliza suala hili kwa sababu Chama cha Siasa ni Chama cha Wanachama na sio cha Viongozi. Hivyo wenye Chama yaani Wanachama wanafahamu kinagaubaga kuhusiana na ndoa hii. Na kama wanafahamu basi hakuna hata mwanandugu mmoja aliyethubutu kutoa tahadhari ya kupima ‘VVU’ wa kisiasa kwanza kabla ya ndoa.

Nina mashaka hayo kwasababu miongoni mwa waliofungishwa ndoa hii mbona wanazo dalili za Virusi vya Ukimwi wa Kisiasa. Narudia kusema mashaka yangu na sio dhambi mwanadamu kuwa na mashaka kwani yananisaidia kuwa mwangalifu. Ukimwi wa kisiasa hauna dawa wala kinga kama Ukimwi ule mwengine. Sasa tutafanyaje wanandoa hawa watakapoambukizana. Si ndio utakuwa mwanzo wa vifo vyao na mwisho wa maisha yao.

Nia yangu ni kuwasaidia na sio kuwavunjia. Kwa maana mimi sina wivu na kati ya yeyote ya wanandoa hawa. Lakini Ukimwi unaua. TAHADHARI kwa wale ambao hawajaoa au kuolewa na hawa.



USHIRIKA MPAKA PEMBA

Tumepokea taarifa ya kuundwa kwa Ushirika wa Vyama vya siasa uliohusishwa Vyama vine kati ya vingi vilivyo katika kambi ya upinzani. Vyama hivi ni CUF, CHADEMA, TLP na NCCR – MAGEUZI.

Siasa za Vyama vingi zilizoanza rasmi hapa Tanzania mwaka 1992 zinatupa picha ya kuwa takriban kila Chama kina eneo lililolidhibiti ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nikitolea mifano, CCM imedhibiti eneo karibu lote la Tanzania, isipokuwa kule Pemba. Ambapo TLP ina wanachama wengi zaidi Kilimanjaro ya Uchagani, UDP Shinyanga hususan Wilaya ya Bariadi.

Katika Ushirika huu ulioundwa pale Buguruni Dar es Salaam tarehe 10/05/2007 Chama cha CUF kimejidhihirisha kuwa katika ndoa hii ndio Chama pekee chenye eneo la kujidai, ambapo tokea uchaguzi wa kwanza wa Vyama vingi mwaka 1995 wamelidhibiti hadi sasa. Eneo hili ni eneo lote la Kisiwa cha Pemba kule Zanzibar.

Tabaan mwaka 2003 ulipofanyika uchaguzi mdogo kwa baadhi ya Majimbo ya kule Pemba na baadhi ya Wagombea wa Chama cha CUFkuenguliwa katika orodha ya wagombea wanachama na wafuasi wao waliamua kupigia kura “maruhani” baada ya wagombea, wa vyama vyengine vilivyogombea. Matokeo ya uchaguzi ule yalidhihirisha umwamba na undava wa CUF ndani ya Pemba. Walioshinda katika Majimbo ambayo hayakuwa na wagombea wa CUF walipata kati ya kura 300 na 1000 miongoni mwa takriban kura 4000 hadi 5000 zilizopigwa. Waliogombea pamoja na CCM walikuwepo waliowakilisha Vyama vya Upinzani na zaidi walikuwa wagombea wa NCCR-MAGEUZI na TLP, ambao sasa ni miongoni mwa wanandoa/wanaushirika huu ulioundwa.

Wana haarakati wa masuala ya kisiasa hapa ndipo wanapouliza masuala yao kuhusiana na Ushirika huu. Je kweli kwa makubaliano haya, Chama cha CUF watakuwa tayari kuachia sehemu ya Majimbo yake ya Pemba kwa TLP, CHADEMA au NCCR – MAGEUZI, ili kuimarisha upinzani kule Zanzibar na kujenga nguvu za pamoja za kupambana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na CCM Zanzibar. Kama hii itawezekana na tunaomba Mwenyezi Mungu iwezekane litafungua ukurasa mpya katika harakati za kisiasa nchini na litadhihirisha upevu wa kisiasa kwa viongozi wa Vyama hivi. Lakini endapohili halitawezekana na hatuaombi iwe hivyo, litathibitisha ule usemi wa Kiswahili usemao “CHAKO CHETU, LAKINI CHANGU CHANGU”. Hali hii siyo tu italeta ufa katika ushirika huu bali utakuwa mpasuko na mwisho wa ushirika.

Kuwa kuwa ushirika huu umeshatiwa sahihi na kubarikiwa na Vyama hivi, tunafikiri pahala pazuri pa kuanzia kudhihirisha nia njema ya viongozi hawa katika kushirikiana wasisubiri mwaka 2010 au kuweka shinikizo la mabadiliko ya Katiba na Tume ya Uchaguzi. Bali Chama cha CUF kupitia kwa Kiongozi wake ndani ya Baraza la Wawakilishi apeleke mapendekezo ya Makada kutoka TLP, CHADEMA na NCCR – MAGEUZI kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ili miongoni mwao wateuliwe kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika nafasi kumi za Rais. Hili likifanyika na ni vyema likafanyika sasa litajenga mshikamano wa dhati ndani ya ushirika huu.

Vinginevyo badi hatubaki na mashaka yale yale ya kwambva “chako chetu, lakini changu changu”.

Wakiweza kufanikisha hili la mashirikiano ya dhati, watatuthibitishia kuwa ushirika huu ni kwa Jamhuri nzima ya Tanzania ikiwemo na Pemba. Lakini ikifanyika vinginevyo itakuwa ushirika bila ya kuhusisha Pemba. Na kwa maana nyingine ushirika mwisho Nungwi.

Tunawatakia kila la kheri. Lakini tuanze sasa tusisubiri mwaka 2010.

KILEMBA CHA UKOKA

TUNAWAAOMBIA CUF WAACHE KUMVISHA KILEMBA CHA UKOKA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO MHE.JAKAYA MRISHO KIKWETE
Ni kweli dunia ina vituko. CUF baada ya kumkejeli Rais Kikwete wakati wa Uchaguzi Mkuu, leo wanamwendea kumuomba awasaidie ili aandae mazingira yatakayowezesha kuundwa Serikali ya mseto Zanzibar. Viongozi wa CUF waliyoshindwa na CCM, wapewe nyadhifa za juu Serikalini kwa kile wanachokidai kuondoa mpasuko wa Kisiasa. CUF hawamjui Rais Kikwete na wahenga wamesema “Jambo usilolijua ni usiku wa kiza”. Si dhani kwamba itakuwa jambo la rahisi kwa Mhe. Rais Kikwete kukubali matakwa yao. Hivi karibuni Wana CCM Zanzibar walifanya maadhimisho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mmoja wa ushindi wa CCM uliopatikana katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 30, 2005. Kwenye maadhimisho hayo wamempongeza Rais wao Mhe. Karume. Naye amepokea pongezi hizo kwa furaha na bashasha kubwa. “Tunaendelea kwenye shughuli muhimu za kujiletea maendeleo yetu kwa faida ya wote bila kujali Itikadi za kisiasa. Mabarabara, nyumba, Mashule, Hospitali na tunaendelea kuimarisha Uchumi wetu kwa kasi isiyo na kifani kupitia Sekta mbali mbali”. Alisema Rais Karume kwenye mkutano huo wa kujipongeza.

La kushangaza ni kwamba Viongozi wa CUF baada ya kuona ukweli kwenye maendeleo yetu wameamua kwenda kumuona Rais wetu mpendwa Mhe. Kikwete, eti awasaidie kubatilisha Ushindi wa CCM kwa kile wanachokiita “Uchaguzi sio huru na haki” na kwamba CCM imefanya udanganyifu – imepora ushindi wa CUF. Jee hilo linakubalika au janja yao?

Tunawaambia CUF watambue kuwa hilo haliwezekani. Wasijigambe kutaka kumvisha kilemba cha ukoka Rais wetu. Hivi juzi kwao alikuwa ni kiongozi asiye na uwezo, leo awe na uwezo wa kukiuka Katiba ya CCM na Serikali zake kwa kubadili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iwe ya Mseto wa CCM na CUF? Hilo ni kujidanganya kupita kiasi.

Sisi tunafahamu fika ujanja wa CUF kuwa ni urithi wa asili wa Chama Cha Hizbu na bwana wao Sultani. Hizbu yaani ZNP ilikuwa daima dawamu haikubali ushindi wa ASP. Katika chaguzi zote zilizo fanyika takriban mara nne hapa Zanzibar tangu 1957 – 1963, kwa mizengwe na ukaidi wa Hizbu, ASP ilishinda karibu katika chaguzi zote hizo, lakini ushindi haikupewa.

Lakini hata baada ya nchi yetu kurejea katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwanzo chini ya Demokrasia hii mwaka 1995 na 2000 na wa mwaka 2005, CUF haijakubali kushindwa pamoja na kwamba mara zote hizo wameshindwa kweli kweli. Kiongozi wa CUF Seif Sharifu Hamadi hajapata kukubali kushindwa mahala popote alipogombea. Kila Uchaguzi unapofanyika akishindwa anadai urejewe tena eti alifanyiwa mizengwe.

Majuzi Wabunge wa CUF walitaka kueleza maelezo hayo hayo ndani ya Bunge. Sasa kwa kuwa wanaona Chama chao (CUF) kila uchao kinadidimia, hakina pa kushika wanabuni mbinu za kuwatuliza wafuasi wao wasisambaratike.

Baada ya kushindwa na CCM katika Uchaguzi uliopita, sasa wameamua kuwmendea Mhe. Rais Kikwete kumuomba amshawishi Mhe. Amani Abeid Karume aunde Serikali ya mseto kwa Zanzibar. Seif ameashau kwamba Rais Kikwete alitaraji kuungwa mkono na wafuasi wa CUF Pemba pamoja na kuwa na wafuasi wake wengi Unguja na Tanzania Bara. Hilo hakuliona, wakati ule alimsema kuwa ni Rais asiye na uwezo, akidai kuwa yeye na Lipumba ndio wanaofaa zaidi.

Jee, leo Seif kumpigia magoti Rais Kikwete huoni aibu? Ndipo kwa sisi Wana CCM tunateta kua anamvisha kilemba cha ukoka Rais wetu. Hilo haliwezekani wala halivumiliki kwa upande wa Wana CCM.

Katika tamko walilotoa viongozi wa CUF wamesema kuwa wanamuunga mkono Rais Kikwete kwa matamshi yake kuwa atashughulikia mpasuko wa Kisiasa Zanzibar kwa dhana kwamba ataifanya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iwe ya mseto na hivyo CUF kumuona Rais Kikwete kuwa ni Mkombozi wao.

Sisi Wana CCM, Wakereketwa na Wapenda amani tuliopo Zanzibar tunaona kama CUF wanacheza mchezo wa kitoto kwa kudanganyana. Maana sasa Uchaguzi umekwisha, Serikali zimeshaundwa na zinafanya wajibu uliokusudiwa. Kilichobaki sasa wana CCM na Wana CUF ni kushirikiana vizuri katika ujenzi wa Taifa letu sio kusubiri mseto. Huo ndio uzalendo unaohitajika sasa. Pale wanapoona pana makosa wasaidie kukosoa kwa maslahi ya Taifa badala ya kusubiri iundwe Serikali ya mseto. Tunawaambia wana CUF kwamba Uchaguzi uliopita umekwishapita hivyo wajiandae kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, maana Katiba ya Tanzania inatamka kuwa Uchaguzi Mkuu utafanyika kila baada ya miaka 5. Tunasema tena kwamba haifai wana CUF msijidai kumvisha Rais wetu kilemba cha ukoka.

“MAPINDUZI DAIMA”

“MSETO ZII”

AHADI HEWA ZA CUF

WALIOCHOSHWA NA UONGO NA KUSUBIRI AHADI HEWA WAIHAMA CUF NA KUJIUNGA NA CCM PEMBA

Subira ni neno la Kiswahili lenye maana pana sana, ni kusubiri, kustahamili, kuvumilia, kungoja kwa muda mrefu sana. Lugha nyingi zimetoa methali zenye mnasaba na neno hili. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili kuna methali zisemazo “Mwenye kusubiri hajuti. Mstahamilivu Hula Mbivu. Subira yavuta kheri. Ngoja ngoja yaumiza matumbo”, ubira ni ufunguo wa peponi”.

Na katika lugha ya Kiarabu pia uko msemo ambao tafsiri yake kwa Kiswahili unasema “Hakika Mwenyezimungu yupo pamoja na wenye kusubiri”.

Pia kuna washari walioimba mmoja namkumbuka yeye alisema katika ushairi wake:-

“Nimesubiri zamani Kama ulivyonitaka
Na mengi nikajihini Ingawa na dhulumika
Kukuridhi Muhisani Hadi uliporidhika”

Mshairi huyu katika kibwagizo chake kwenye ushairi wake huu aliendelea kusema.

“Tena hakika wajua Subira ina mipaka
Watu wengi hujiua Subira ikiwatoka
Ni ngumu kuvumilia Wachache wanaovuka
Sijashindwa nnaari Japo ni ngumu subira
Nitazidi Kusubiri Sitoifanya papara”.

Hiyo ndiyo subira, stahamala na uvumilivu, na kadri nitakavyoieleza mwisho tutakuta kuwa subira, ustahamilivu na uvumilivu vyote vina mwisho. Kuna wengine utawasikia wanasema “Stahamili joto la Bekari upate Mkate”. Hebu tujiuleze! Hivi kweli binadamu anaweza kukaa kwenye tanuri la kuokea mikate kwenye bekari kwa muda wa siku ngapi asichoke? Jawabu yake kwa muda wa masaa tu ataamua kuodoka kama hajaupata mkate. Hatimaye atasema kama mateso yenyewe ni haya, ni bora kuukosa, ataamua kuusamehe.
Dhana ya subira na uvumilivu ina mashaka yake, kwani inategemea na mazingira kile unachokisubiri. Kwani wahenga wanatwambia! “Ukiisubiri iliyokwishakuiva utakula mbovu”. Na ukisubiri iliyopooza utakula iliyooza” Methali nyengine ya wahenga inasema! “Ngoja ngoja yaumiza matumbo”, kwani tumbo lenye njaa halina subira.

Tunaamini wengi wa wale wanaoamua kusubiri, huwa wana Itikadi ya Dini na wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa kutokana na subira yao watalipwa huko Akhera siku ya hesabu. Na huwa wanasubiri tu hawalalamiki wala kunung’unika, kwani wanaamini kuwa wakifanya kinyume chake hawatapata malipo huko Akhera.

Na kuhusu uongo je?
Sisi tulipokuwa wadogo tulikatazwa sana kusema Uongo, uongo maana yake ni kusema jambo ambalo halipo si la kweli ni “Uzushi”. Ni matusi makubwa mtu mzima kuambiwa muongo. Tulipokuwa wadogo tuliambiwa kuwa adhabu ya mtu muongo kesho siku ya kiama atavutwa ulimi mpaka ufikie pima saba. Ambapo pima moja kwa vipimo vya sasa ni kama mita mbili. Halafu mtu muongo kesho Akhera atapigwa marungu ya moto. Na hatimae kuchomwa moto.

Waswahili wanasema “Muongo Muongoze” na “Njia ya Muongo ni fupi” chambilecho bibi yangu mlezi Mwana binti Hadidi siku zote alikuwa akinambia “Ukisema uongo lazima uwe na kifuniko”. Nilikuwa simuelewi alikuwa akimaanisha nini wakati ule. Kumbe maana yake, uongo wangu nisiutoe nje watu watautambua tu. Na kwa falsafa yake anamaanisha kuniambia kuwa nisiseme uongo. Kwani “Kweli itakapodhihiri uongo utajitenga tu”.

Yupo mwanafalsafa mmoja alisema “Huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote, bali utawadanganya baadhi ya watu na kwa baadhi ya wakati tu.”

Kuna matapeli wa kisiasa waliwadanganya wananchi wa Zanzibar hasa katika kisiwa cha Pemba kwa muda usiopungua miaka 15. viongozi hawa wa CUF waliwaambia watu uongo mchana, kuzimu hakuna nyota, tena uongo wao chambilecho bibi yangu ulikuwa hauna hata kifuniko.

Waliwaambia wananchi wa Pemba eti kuwa CCM haijafaanya kitu chochote cha Maendeleo tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Walisema ni bora Ukoloni wa Kisultani kuliko utawala wa CCM. Hakuna haki wala Uhuru katika nchi. Walidanganya kuwa eti ikitawala CUF bei ya kilo moja ya mchele itauzwa Tshs. 50/= , litajengwa daraja kutoka Mkoani Pemba hadi Nungwi Unguja. Eti wananchi watatoka Pemba kwenda Unguja kwa gari badala ya Boti na Meli. Almuradi waliwadanganya baadhi ya wananchi wa Pemba na wakadanganyika.

Lakini kama ilivyo kawaida kuwa, hutaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati wote, bali utawadanganya baadhi ya watu tu, tena kwa baadhi ya wakati. Hili linathibitika kwani sio wananchi wote wapemba waliokubali kudanganywa na CUF wengine walikataa, na hao baadhi ya waliokubali kudanganywa, sasa wameanza kung’amua.

Hali hii inadhihirika kutokana na tukio lililojitokeza mwishoni mwa mwezi wa Juni mwaka huu ambapo wanachama wa CUF 54 wa kijiji cha Matungu Shehia ya Vitongoji Jimbo la Wawi Chake Chake Pemba waliamua kwa hiyari yao kuishusha bendere ya CUF katika tawi lao. Waliungoa mlingoti wa bendera wa jiti na kweka mlingoti mpya wa chuma na hatimae kupandisha bendera ya CCM, na wao wenyewe wote wakajiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Siku ya Jumapili iliyopita tarehe 1/7/2007 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Saleh Ramadhan Ferouz alikwenda kuwakabidhi kadi za uanachama wa CCM wananchi 54 walioamua kwa hiyari yao kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Wakati anapokewa na mamia ya wananchi wa kijiji hicho kwa shamra shamra ya aina yake iliyoongozwa na Dufu! Mhe. Ferouz aliwauliza. Je, mmeamua kuishusha bendera ya CUF kwa hiyari yenu? Walijibu “Ndiyo kwa hiyari yetu. Na mmeamua kujiunga na CCM kwa hiyari yenu? Walijibu “Ndiyo kwa hiyari yetu. Na alizidi kuwauliza. Hamkushawishiwa na mtu yeyote? Walijibu “Ndiyo hatukushawishiwa na mtu yeyote.

Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wananchi. Wanachama hao walieleza sababu za kufikia uamuzi wao wa kukiacha chama cha CUF na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi. Ni kuwa wamechoka kudanganywa na viongozi wa CUF kwa kupewa ahadi hewa za kesho kesho ambazo hazitekelezeki. Aidha walisema kuwa wao wanataka maendeleo na wanaamini wakiwa ndani ya CUF hawatapata maendeleo.

Walisema, wamesubiri kwa muda wa miaka kumi na tano (15) wakiwa ndani ya CUF kijiji chao hakikupata maendeleo yoyote. Wamebakia kuwa hawana umeme, maji safi na salama, zahanati wala barabara. Lakini ndani ya siku saba tu, baada ya uamuzi wao wa kukihama cahama cha CUF na kujiunga na CCM, tayari kijiji hicho kimekwisha pata umeme na wameahidiwa kuwa Zahanati yao itamalizwa hivi karibuni, barabara na maji safi vinafuata pia.

Katika risala yao waliyoisoma katika mkutano wa hadhara mbele ya Naibu Katibu Mkuu Mhe. Saleh Ramadhan Ferouz walieleza kuwa wameamua kujenga jengo jipya lenye hadhi ya Chama ambalo litatumika kama afisi ya CCM ya Tawi lao, ambapo wenyewe wamepima kiwanja na kukusanya matufali, chokaa na mawe. Katika kuunga mkono juhudi zao, hapo hapo ulianzishwa mchango na kupatikana jumla ya Tsh 360,200/- (laki tatu na elfu sitini na mia mbili) wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar yeye binafsi na familia yake amechangia T Sh 100.000/-
Mwenyekiti wa Tawi mama la CCM Ng’ambwa amechania Sh 50,000/-. Mama Shadiya Karume amechangia mifuko 25 ya saruji.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ambapo yeye alichangia Tsh 50,000/- kwa niaba ya Jimbo lake la Mpendae.

MWNYEKUPINGA NEEMA ZA MOLA II

MWENYE KUPINGA NEEMA ZA MOLA NI KAFIRI

MWAKA 2005, Watanzania tumeshuhudia nchi yetu ikifanya Uchaguzi ambao ulikuwa wa amani na utulivu, Uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza wakaguzi wa kitaifa na kimataifa walikuja kushuhudia hali halisi ya Uchaguzi huo ulivyoendeshwa. Waangalizi hao walikiri kuwa Uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki pamoja na kwamba palikuwa na kasoro ndogo ndogo (mapungufu) za hapa na pale ambazo hufanywa na kila binadamu ye yote duniani.

Pamoja na kuwa huru na wa haki, lakini pia ni Uchaguzi uliokuwa na vitendo vingi vibaya vilivyotokea wakati wa Uchaguzi wa Mwanzo na wa Pili uliohusisha Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa – yaani (1959 na 1963). Hapa Zanzibar, watu kubaguana kwa Itikadi zao za vyama kung’oleana mazao wanachama wa Chama fulani kuitwa Mabunju, Makafiri n.k. na haya yote yaliandaliwa na watu wanao jidai kuwa ni Masheikh, kwani hao ndio wanaojiita Masheikh na Wastaarabu na lakini kila uchao wanadiriki kutangaza Misikitini, kuwa Serikali ya Mapinduzi ni Serikali ya dhulma iliyoiondoa eti Serikali halali ya SAYYID JEMSHID BIN ABDULLAH, BIN KHALIFA BIN HAROUB, Serikali iliyokuwa ikiongozwa na MOHAMED SHAMTE BIN HAMAD.

Aidha, wanathubutu kutangaza hadharani na bila kimeme kwamba kila anayeunga mkono Chama cha Mapinduzi ni kafiri na ataingia motoni kesho huko Akhera. Kwa hali hiyo, napenda kuwauliza Masheikh hao kuwa wamezitafakari vizuri kauli zao hizo?. Wamechunguza kwa makini siri ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla?.

Nachukua nnafasi hii kuwaomba watu wa aina hiyo wayatafakari maelezo ya makala hii na hatimaye waweze kutoa maamuzi muafaka kama kweli wao ni wananchi na hasa wazalendo wa Zanzibar, kufanya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, waliyafanya kwa misingi ya haki au walifanya kwa ajili ya kutekeleza amri kua ya nani?
Siasa za kupigania Uhuru Zanzibar zilianza wakati wa utawala wa SULTAN SAYYED KHALIFA BIN HAOUB, ambaye ni babu yake Jemshid. Ni Mwarabu mwenye asili ya Oman. Kwa desturi ya Waarabu, neno kila neno linafsiri yake au linatokana na matokeo ya jambo/kitu fulani. Sasa tuangalie maana halisi ya neno SAYYED (Bwana), KHALIFA (Mtumwa), HAROUB (Matata au Vita). Ni utawala uliojaa matatizo makubwa na yasiyoweza kuvumiliwa na wananchi wowote duniani.

Hivyo, wakati wa utawala huo, Mwenye-zimungu - Mwenye Uwezo Mkubwa na Mwingi wa Rehema, aliwapa uwezo wananchi wa Visiwa hivi vya Unguja na Pemba waliokuwa wakidhalilishwa, kukandamizwa na kudharauliwa ndani ya nchi yao, ndiye aliyewafumbua macho Waafrika wa Zanzibar na kuanza kudai haki ya kujitawala. Kiongozi aliyejitolea kupigania haki hiyo si mwengine bali ni Hayati ABDEID AMANI. Kwa vile jina hilo ni la asili ya Kiarabu lina tafsirika kama ifuatavyo - ABEID (Abdi yaani Mtumishi au Mjumbe), AMANI (Utulivu). Kwa ufupi, ni majina yenye kupendelea zaidi hali ya amani na utulivu kwa mmaslahi ya wananchi wote na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa majina haya KHALIFA BIN HAROUB na ABEID AMANI KARUME, wote walikuwa ni Watawala katika nyakati tofauti, lakini tutagundua kuwa KHALIFA BIN HAROUB - Mtawala huyu alikuwa na Utawala wa Kidhalim tofauti na mwenziwe ABEDI AMANI - ni Mtumishi au Mjumbe aliyekuja kuondoa utawala wa matata/matatizo na kuweka utulivu kwa wananchi wa jamii ya Wazanzibari, waliokuwa wanayumbishwa na kubaguliwa pasipo na misingi yoyote.

Utawala wa Kisultani uliwagawa Wazanzibari, kwa misingi ya rangi, kabila, dini na jinsia na baya zaidi walitugawa wananchi kwa misingi ya Wapemba na Wazanzibari. Utawala huo uliweka pingamizi kadha dhidi ya Wapemba na Wazanzibari (Waunguja). Mathalan, Wapemba waliotaka kuja Zanzibar, walitakiwa kwanza wapate kibali kutoka kwa Sheha na Mudiri. Akifika tu Zanzibar lazima aripoti kwa Mudiri na kwa Sheha kwa nia ya kueleza ni sababu zipi za msingi zilizomfanya aje Unguja na ataishi kwa muda gani. Kwa hali hiyo, halikuwa jambo rahisi hata kidogo kwa Mpemba kuja Zanzibar ni sawa na kwenda Ulaya.

Mwaka 1954, mama yangu aliolewa Kisiwani Pemba na Bwana Juma bin Nafasi, mkaazi wa Mgelema. Namkumbuka mzee mmoja mkaazi wa Kisiwa hicho, alirejea kutoka Zanzibar. Alipokelewa na wanakijiji hicho cha Mgelema kama vile ametoka Makka, Saudi Arabia. Kina mama walikwenda kumlaki kila mmoja akiwa na mbuzi yake ya kukunia nazi ili kuweza kushiriki kikamilifu katika kukuna nazi zitakazotumika katika kuandaa chakula cha sherehe hiyo ya kumpokea mgeni huyo aliyerudi kutoka Zanzibar. Hakika, ilikuwa ni sherehe kubwa na ya aina yake. Hali hiyo ilisababishwa na utawala dhalimu wa Sultani. Utawala huo uliwafananisha Waafrika wa Zanzibar kuwa sawa na MBWA.

Nakumbuka mnamo mwaka 1953, Jemshid, mjukuu wa Sayyid Khalifa bin Haroub – mtawala wa Zanzibar (wakati huo) alimponda kijana aliyekuwa akiitwa Ali Machano, eneo la Kidongo chekundu karibu na Mental Hospital yaani Hospitali ya watu wa akili (sasa Luncastar). Jemshid bila aibu alitamka hadharani –“huyu Mbwa amechafua gari yangu”.

Sultan aliwafanya Waarabu hasa wa Oman kana kwamba ni watawala dhidi ya Waafrika. Ilifikia hadi kitendo chochote ata kachofanyiwa Muafrika na Mwarabu kina kuwa ni sawa tu. Kuna visa vingi walivyofanyiwa Waafrika, kwa mfano Mwafrika akipondwa na Mwarabu kwa baskeli, badala ya kupewa pole adabu yake anapigwa bakora na matusi juu yake yaani anaambiwa hana adabu sababu unabonde hajui wewe kama baskeli yangu kengele Lucas, Breki Nta fira Danlop sababu unabonde - yaani sababu gani amemponda kwa hivyo Mwafrika huyo hana adabu hajui kuwa Baskeli yake breki ni nta, mpira ni Danlop na kengele yake aina ya Lucas sababu amemponda hana adabu, anapigwa bakora, kupondwa kupondwa na bakora juu madam ni muafrika astahili adhabu hiyo. Wazee wetu kudhalilishwa kuchukuliwa wake zao huku wakiona, Said Sudi akiwakamata wanawake kwa nguvu mbele ya waume zao na kuwapeleka anakotaka na waume zao wakiangalia tu kwa sababu Said Soud ni katika aila ya Mfalme. Kama hiyo haitoshi, Usultani ulikuwa unawadhalilisha hata mayatima. Wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Madrassa ya Sheikh Ameir Tajo, iliyokuwa katika mtaa wa Kwaali Nathoo, mjini Zanzibar, nilikuwa nikiwaongoza baadhi ya watoto yatima kwenda kwa Said Khalifa. Jambo la kusikitisha, kila siku tunayokwenda huko, tukifika nyumbani kwake, tulilazimishwa kupanda ngazi kwa magoti huku tukiimba “Salam Malik Rabbana Bukhlana Sultan Khalifa”. Tunapanda mpaka juu hadi kunako Seble yake (Mfalme). Hapo huja mke wake Bi. MATKA au Mfalme mwenyewe na kuanza kutoa zawadi mbali mbali zikiwemo vitambaa vya kanzu au thamani yake pamoja na wakati mwengine hupata vitambaa vya kanzu pamoja na Tshs. Tatu (3/=) kwa kila mmoja wetu na hatimaye tunarejea kwa magoti mpaka chini na kuondoka. Haya ni theluthi tu kati ya madhila kadhaa niliyoyaeleza ya Utawala ambayo mimi nimeyaona kwa macho yangu yakifanywa kwa makusudi na utawala wa Sayyid Khalifa bin Haroub.

Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba Zanzibar ni kitovu cha Uislamu na Mabingwa wa Lugha ya Kiarabu pamoja na fani ya lugha hiyo. Pamoja na maovu yote yanayofanyika hapa, hakuna hata Sheikh mmoja aliyewahi kutamka kuwa Utawala wa Sayyid Khalifa bin Haroub ni wa Kidhalimu, badala yake Masheikh hao ndio waliokaza kamba kuutetea kwa hali na mali na kutaka kuulazimisha umma wa Wazanzibari utii na umuenzi mfalme. Kwa lipi zuri hadi jamii ilazimishwe hivyo?. Hebu tumwangalie Mwana Mapinduzi Abeid Amani, baada ya kutimiza azma ya jina lake na kufaulu kuigomboa Zanzibar kutoka kwenye utawala huo wa mabavu.

Mara tu baada ya kufanikiwa Mapinduzi matukufu ya 1964, Hayati Mzee karume, aliondosha aina zote za ubaguzi, ubwana na utwana, hakujali mweusi wala mweupe, kabila au dini. Aliubadilisha Mji wa Zanzibar kuwa wa kisasa kabisa, kuboresha mfumo wa elimu hadi leo tunao Maporofesa wa Makabila na jinsia mbali mbali. Aliweza kubadili maisha ya wanyonge wote wa unguja na Pemba. Mathalan, Watumbatu wa leo sio wale wa enzi za Kiusultani waliokuwa wakitumwa kulima katika mashamba ya Mabwana wa Kiarabu, Wahindi n.k. Aidha, jamii ya Wazanzibari wa leo sio ile ya jana. Jamii ya leo inauelewa mkubwa wa mambo na kwamba wanajua hata kufanya biashara sawa na wale wa jamii ya Asia (Wahindi).

Iweje leo Masheikh “Vilemba” hao wathubutu kusema eti Utawala wa sasa una kwenda kinyume na Maadili ya Uislamu. Sina haja ya kusema chochote kuhusu hili, bali naomba kuwauliza Masheikh wa aina hiyo kwamba kila Chuo Cha Kiislamu Cha Muslim Accademy kilichokuwa na zaidi asilimia sitini (60 %) ya mashoga asilimia 60, Ule ndio uiwslamu? Nani asiyejuwa kuwa Mkamasini na Mlango wa Chuma palikuwa na Madanguro?. Jee, kuna Sheikh yeyote miongoni mwa hao tunaowazungumza aliyewahi kukanusha?.

Kama kweli wanapenda haki basi hawana budi kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Uadilifu wake mkubwa wa kuondosha maovu yote ya kikoloni yaliyokuwa yanafanyika nchini humu kwa makusudi na bila ya woga wowote. Aidha, wanapaswa kumuombea dua la kheri Marehemu Mzee Karume, lakini kwa ukosefu wa fadhila na kwa unafiki walionao ndani ya nafsi zao, walizidisha fitna pamoja na kupandikiza mbegu za chuki, zenye chembe chembe za dharau na kupambwa na joho la ufedhuli, kejeli na kebehi dhidi ya Mwana Mapinduzi huyo. Kama hiyo haitoshi, bila ya halali na kwa chuki zenu wapinga maendeleo wa Taifa hili walidiriki kumuua Mzee wetu huyo (Karume). Lakini kifo cha Mzee Karume kama Masheikh wanafiki wagekuwa wanafahamu, wanapaswa kutafakari kwa upeo zaidi majina ya viongozi waliofuatia baada ya kifo cha Mzee Karume, kwani mdorongo wa majina ya viongozi hao yanayotoa sura halisi ya kiungwana. Pamoja na ukweli kwamba Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoandaliwa na kuongozwa na Mzee Karume, lakini kwa kweli Mapinduzi hao yalipangwa na Mwenyezi Mungu (Subuhanahu Wataala).

Wadhalimu baada ya kumuua Mzee Abeid Amani Karume walidhani wamefanikiwa kuangamiza dhamira ya Mapinduzi, kumbe Mwenyezi Mungu amewapa mtihani wapinga maendeleo hao ili wazingatie na kutafakari kwa nini Mola baada kuuawa Mzee Karume, kamleta Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ?. Kwa ufupi , tafsiri yake ni kwamba neno “Aboud” ni mtiifu au kufuata amri. Neno hili amelitumia Mola kwenye Aya Wamakhalaka–ljini wal-insi ila liabudullah – maana yake ni kwamba “sikuwaumba watu na majini ila wanitii. Kwa maana hiyo, Aboud Jumbe ni mtiifu wa Mjumbe yaani wa yale yaliyoachwa na Mjumbe wa Amani. Mafisadi walikwisha jipenyeza ndani ya Serikali ya Mapinduzi, wakala njama za makusudi za kutaka kumtoa Mzee Aboud Jumbe, kwenye madaraka ya Urais wa Zanzibar, ili mafisahdi hao wapate kutwaa madaraka hayo kiurahisi. Mwenyezi Mungu kwa hekma zake, akatupa somo Wazanzibari sote na hatimaye akatuletea kijana mwengine mpya kabisa na mwenye uchungu na Taifa hili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, ili kuchukua nafasi iliyowachwa na Mzee Jumbe.

Kama kawaida, neno Ali maana yake ni muadilifu. Hassan (mwema). Hapa Mola, anatukumbusha uadilifu pamoja na wema aliotufanyia huko nyuma (1964), nasi tukaitikia amri yake na tukawa tayari kwenda “Bomani” na hatimaye kupindua Serikali ya kikoloni hali yakuwa hatuna silaha ya kuaminika. Tumeingia Bomani humo tukiwa na mapanga, mawe na mishale, huku tukijua Bomani kuna bunduki, mizinga na silaha nyengine nzito zaidi na hivyo kuifanya Zanzibar kuweka historia ya aina yake duniani kwa kufaulu kuung’oa utawala wa kisultani kutokana na maandalizi duni nay a muda mfupi mno.

Kuja kwa Rais Ali Hassan, ilikuwa ni ukumbusho na kututahadharisha Wazanzibari kwamba maadui bado wamo ndani ya Serikali na kila uchao wanafanya njama za hujuma dhidi ya Serikali. Kwa upendo wa Mola juu ya waja wake wa Visiwa vya Unguja na Pemba, ametujaalia maajabu makubwa. Utawala wa Mzee Ali Hassaan, ulichukua muda mdogo. Hii ilithibati tosha kuonesha kwamba alikuja kutoa hadhari juu ya maadui hao wa Mapinduzi ya Zanzibar. Ithibati ya usema huu, unatokana na vitimbwi alivyokabiliana navyo aliyekuja kushika Wadhifa huo Mzee Idrissa Abdul- Wakil, baada ya Rais Ali Hassan Mwinyi, kuachia madaraka.
Mzee Idrisha Abdulwakil nafikiri bila ya shaka wale wataalum kwa lugha ya Kiarabu pamoja na Masheikh na Masheikh wanafanya nini maana Abdul-Wakil, Abdul-Wakil maana yake ni Mjumbe wa kudhukuru kwa maana hiyo Mzee Idrisa Abdul-Wakil ndie kiongozi aliekuja kutoa hokum nani mbaya na nani mwema ndani ya Serikali ya Mapinduzi. Kila mnafiki aliyejitokeza kutokana na hali hiyo, Mzee Idrissa Abdulwakil, alikuwa wakati wote anatimiza kazi yake kwa kutoa hokum dhidi ya wanafiki wote waliojitokeza katika Serikali yake. Hali hiyo iliendelea hadi kufikia muda fulani alipolazimika kulivunja Baraza la Mawaziri na kuwatoa wanafiki wote waliokuwamo ndani ya Baraza hilo. Hakika, Mzee Abdulwakil, ni Kiongozi wa Kwanza kabisa katika Jamhuri ya Tanzania, kuvunja Baraza la Mawaziri. Ukweli usiofichika wale wote aliowafukuzwa kutoka Baraza hilo, ndio hao sasa wamekuwa wapinzani wakubwa wa Serikali (SMZ) pamoaja na Taifa la Zanzibar. Mbaya zaidi viongozi hao wakishirikiana na Masheikh (vilemba) ndio walio mstari wa mbele kupinga na kudiriki kutoa kauli hadharani na bila ya woga kwamba Mapinduzi ya Januari 12, 1964, sio halali wanafiki.


Baada ya kuondoka mzee Abdulwakil, nafasi yake ilichukuliwa na Dk. Salmin Amour (Komandoo). Maana halisi ya neno “Salmin” ni salama mara mbili na “Amour” yaani Amrisha. Itakumbukwa kuwa Rais Salmin Amour, ndie aliyekubali kuanzisha mfumo wa vyama vingi, mfumo ambao maadui waliutaka na kuukaribisha kwa hamu kubwa kwani waliona kuwa wataweza kuutumia mfumo huo kama njia yao yamkato ya kutekeleza azma yao ya kurejea katika utawala wa Kibaraka. Siku ya mwisho ya Kampeni mwaka 1995, kiongozi mmoja wa kundi hilo, alitamka kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Demokrasia (sasa Kibanda Maiti), “eti utawala wa mtu mweusi mwisho leo”. Lakushangaza ni kwamba aliyetangaza kauli hiyo, ni mtu mweusi kama au kuliko makaa (mkaa).

lakini baada ya MOLA kuzima njama zao, walifunga safari kwenda huku na huko duniani, eti kuutaka Ulimwengu uzuie misaada ya kibinadamu kwa Serikali (SMZ), ili jamii ya Waza Zanzibari, iweze kuangamia kwa shida mbali mbali ikiwemo njaa. Kwa uwezo wa Mola (Subhanahu wataala), Mhe. Dk. Salmin (Komandoo), alipambana na njama zote hizo na hatimayejahazi ( Taifa) alilivusha salama. Dk. Salmin alifanya hivyo kwa nguvu zake zote, kwani pamoja na ukweli kwamba hiyo ndio kazi yake lakini kubwa zaidi alifanya hivyo ili kulinda Mapinduzi ya Zanzibar kwa maslahi ya Taifa na watu wake. Wakati huo, mara nyingi, Rais Salmin, alikuwa akiwaliwaza wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba kwa kauli nzuri “tulieni, tulieni, Mola ataleta kheri yake dhidi yetu”. Alikuwa akiwapoza Wazanzibari wakati kauli za mafisadi hao pale alipoona kauli zao zinaashiria shari.

Muda wa Dk. Salmin Amour, ulipomalizika, Wadhifa huo umekamatwa na Rais Aman Abeid. Bila ya shaka tafsiri ya majina haya Masheikh wanayafahamu. “Amani” ni Utulivu na “Abeid” (Mjumbe). Hapa tunakumbushwa kuwa Amani na Utulivu wa nchi hii aliyotuletea Hayati Abeid Amani, kwa uwezo wa Allah, hatuna budi kuulinda kwa nguvu zetu zote. Aidha, tukichunguza kwa makini tutagundua kuwa kazi nzuri aliyoiacha Mzee Abeid, sasa inatekelezwa na Rais Amani Abeid Amani Karume. Lakini si hayo tu, bali tunakumbushwa wema tuliofanyiwa Wazanzibari na Mola wetu kupitia kwa Mzee Abeid Amani Karume. Tunafahamishwa kuwa hao Masheikh vilemba hawafahamu kuwa Wa-Afrika wa Zanzibar waliteswa, kunyaanyaswa na kudharauliwa? Hatupawi kugeuka kama walivyogeuka Mayahudi, kukejili neema walizoteremshiwa na MOLA WETU MTUKUFU AZZA WA JALAH. Tukifanya hivyo, nasi tutaangamizwa kama walivyofanywa Mayahudi.

Jamii ya Wazanzibari na hasa wananchi wapenda amani wote, inajua kwamba wapinga maendeleo hao wameenea kila pembe za Visiwa vya Zanzibar, ili kueneza unafiki wao. Baada ya kuona hawajafanikiwa, hivi sasa wameanza kuleta fitina ya kutugawa kwa kutumia hoja ya Muungano eti si halali na kwamba haukutiwa saini yoyote baina ya Hayati J. K. Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume. Jamii ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla, wanajiuliza nini faida watakayoipata iwapo Muungano huo ukivunjika ?. Aidha, watafanikiwa kuiondoa Serikali ya Mapinduzi ya Unguju ?. Hakika huko ni kujidanganya.

Tunawaambia kuwa Muungano wa Tanzania haukuanza mwaka 1964 kama wanavyofahamu. Muungano wa Tanzania umeanza kabla ya kuingia Mjerumani Mrima na Zanzibar, ilikua ni nchi moja. Hivi hawafahamu kwamba Mjerumani ndiye aliyewatenganisha wa Mrima na wa Zanzibar ?. Waangalie watu wa Mrima na wa Zanzibar, kisilka, kimila na kiutamuduni – hakika zinafanana. Watu wake wanauhusiano wa damu. Mfano mzuri - watu wa Bumbwini na wale wa Kipumbwa huko Tanga walivyokuwa na udugu wa damu. Aidha, watu wa Kizimkazi na watu wa Mafia, Dole na Waruguru, n.k. Hivi hawajui watu wa Makunduchi walikuwa wakicheza Benbati, ngoma yenye asili ya Wanyamwezi ?. Ngoma ya Msondo huchezwa na kinamama wa Kilwa na hata wale wa Tanga, Mtwara ?.

Pamoja na hayo, lakini kuna jambo moja ambalo linaagusa Wazanzibari na Watanzania wengi nalo sio jengine bali inasemekana kumejitokeza kundi jengine la watu (Masheikh) linalojiandaa kuhoji kuhusu Pemba na Zanzibar, eti ilikuwaje ikawa nchi moja ?. Kikundi hiki ni sawa na kile kinahoji Uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Lengo lao ni kutaka kuzima NURU YA MWENYEZI MUNGU KWA VINYWA VYAO. Tunasema hawatafanikiwa, kwani Mwenyezi Mungu anawafahamu vyema wanafiki. Namalizia usemi wangu kwa kuwafahamisha hawa Masheikh vilemba kuwa pamoja na uadui walionao dhidi ya Mapinduzi ya Zanzibar, wajuwe Mapinduzi hayo yametayarishwa na kusimamiwa na Mwenyezi Mungu. Ni yeye ndie anayeyalinda na kuyadumisha milele. Kuhusu Muungano wa Tanzania nao pia umeletwa kwa uwezo wake na kwamba kwa baraka zake atausimamia na kuhakikisha kuwa hautavunjika kwa njama za mafisadi hao. Kwa hali hiyo tunapaswa kuamini kuwa hiyo ni neema iliyoletwa na Mola juu yetu na hivyo yeyote mwenye kupinga neema ya Mwenyezi Mungu ni sawa na Kafiri.
“MUNGU IBARIKI TANZANIA”
“MUNGU IBARIKI ZANZIBAR”

MWINYIHAJALI KONDO/ALI NDOTA - ZANZIBAR.

USHINDI WA 2005

Ushindi 2005 Zanzibar hautopatikana kwa jazba

Wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiendelea kwa kasi, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeshajitangazia kushinda kiti cha Urais Zanzibar hata kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika. Mwandishi Wetu ALLY MWINYIKAI anabainisha iwapo ni vyema kufanya hivyo au la, endelea…

Nadharia ya chama kushinda ina maeneo mapana na kwa kweli ni safari ndefu sana. Mbali ya kuhitajika kuwepo maandalizi ya kutosha lakini kunatakiwa kufanywa tathmini ya hali ya juu katika kila hatua inayochukuliwa katika kuelekea kwenye uchaguzi wenyewe.

Moja ya hatua ya kwanza na muhimu kuliko zote ni uandikishaji. Uandikishaji wapiga kura ni muhimu kuliko jambo lolote jengine. Umuhimu wa jambo hilo kwa Zanzibar ulianza kuonekana waziwazi tangu uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi nchini uliofanyika mwaka 1995.

Umuhimu huo ulijitokeza baada ya kubainika kasoro kubwa zilizofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) upande wa Zanzibar. CCM kilijiamini sana kwa kuwa na wafuasi wengi na hata kubweteka kwa kutotilia uzito unaostahili suala la kuhimiza wafuasi wake kujiandikisha.

Chama hicho kilionekana kutosheka na wingi wa wafuasi iliokuwa nao ambao wakijazana katika mikutano ya hadhara hadi kufikia kutunga nyimbo maalumu iliyokuwa ikisema, “CCM watu kibao.”

Hiyo ni kasoro ambao haijapata kuzungumzwa hadharani kwa karibu miaka 10 sasa, lakini ilikiathiri kwa kiasi fulani chama hicho kwa kuruhusu ushindani wa kisiasa kuonekana mkubwa Zanzibar kuliko sehemu nyingine za Tanzania.

Watafiti wa mambo ya kisiasa Zanzibar walichunguza kutaka kufahamu kwa undani mambo yaliyosababisha chama hicho kupata ushindi mwembamba katika uchaguzi huo licha ya kuwa na wafuasi wengi.

Ugunduzi wa utafiti wao ulibaini mambo mengi ya ghilba na hadaa yalizofanyika ambayo nayo hajatangazwa mahala popote. Miongoni mwa mambo hayo ni wafuasi wa CUF kisiwani Pemba kujifaragua watakavyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu kuruhusiwa kupiga kura zaidi ya mara tatu.

Sehemu moja ya ugunduzi huo ni kuonekana kwamba kulikuwa na kundi kubwa la vijana la wafuasi wa CCM lililohamasika sana wakati wa kampeni za uchaguzi huo lakini lilikuwa halikujiandikisha.

Ilikuwa ni dosari ambayo ilirekebishwa katika uchaguzi uliofuata wa 2000. Kurekebishwa kwa kasoro hiyo kulitoa nafasi ya baadhi ya wachambuzi waliokuwa hawakuvutwa na hisia za kisiasa za upande mmoja kutabiri mapema nani angeibuka mshindi katika uchaguzi huo.

Hapana shaka, matayarisho ya uandikishaji wapiga kura katika uchaguzi wa 2000 yalidhihirisha wazi kwamba CCM ingeshinda na hata wapinzani walioshiriki uchaguzi huo waliuchukulia uchaguzi huo kwa tahadhari kubwa. Tahadhari hiyo ndio mara ilipopatikana fursa ya kugomea, CUF waliitumia ipasavyo.

Ni katika uchaguzi huo, Chama cha Wananchi (CUF) kilisusia kushiriki katika uchaguzi wa majimbo 16 ya Mkoa wa Mjini/Magharibi, hapana shaka kwa kuelewa kwamba hakukuwa na mwanya wa chama hicho kushinda zaidi ya kuendeleza wimbo wake wa kuibiwa kura.

Hakukuwa na njia nyingine ya CUF kufanya katika uchaguzi huo hasa kwa kuzingatia kwamba chama hicho kilikuwa kimeshawaahidi wafuasi wake kushinda katika uchaguzi huo kutokana na tamaa iliyokuwepo kwa kuangalia ushindi mwembamba wa uchaguzi wa 1995.

Kauli za chama kimoja kutamka kushinda na baadaye kugeuza kibao cha kuibiwa kura inaonekana kuanza kuota mizizi hivi sasa kutokana na kusikika kwa matamshi ya kushinda katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu. Kauli hizo zimeshatolewa na viongozi wa CUF.

Matamshi ya viongozi hao kwa kiasi kikubwa yameanza kuvuta hisia za wafuasi wa chama hicho kwa kuyaamini na hasa wafuasi wasiokuwa na nyenzo za kufanyia uchambuzi wa kina juu ya masuala ya siasa na mwenendo mzima wa uchaguzi unavyokuwa.

Kitu kikubwa kinachoangaliwa katika uchaguzi wowote ni idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura na wanaoshiriki katika zoezi hilo siku ya uchaguzi yenyewe. Wakati viongozi hao wa CUF wanajitangazia ushindi wanaelewa wazi kwamba ni watu 157,343 Pemba na watu ……. wameorodheshwa Unguja kwenye daftari la kudumu la wapiga kura la Zanzibar.

Wasiwasi huo unakuja kwa kuangalia nguvu za vyama vinavyotegemea kushiriki katika uchaguzi huo na maeneo ambayo vyama hivyo vina ngome zao. Hapana anayepinga kwamba CUF inawafuasi wengi katika kisiwa cha Pemba ikilinganishwa na CCM ambayo ngome yake kubwa iko Unguja.

Hivyo, kinachoonekana katika jitihada za wanasiasa kujitangazia ushindi ni kutaka kuendeleza hisia za kuvuruga mawazo ya baadhi ya wafuasi wa vyama na kuanza kujiwekea kinga mapema ili matokeo yatakapokuwa kinyume na matamshi ya awali kujengwa dhana ya kuibiwa kura.

Historia inaonesha chanzo cha machafuko ya kisiasa ya hivi karibuni kilitokana na CUF kujitangazia ushindi mwaka 1995 kupitia idhaa moja ya Televisheni hapa nchini kwa kutoa matokeo ya kubuni. Kutangazwa matokeo halisi suala la kuibiwa kura ndipo lilipoibuka na vurugu kuenea.

Muafaka uliofikiwa kati ya vyama vya CCM na CUF unatanabahisha kuepukwa jazba zinazochochea chuki na uhasama pamoja na kusisitiza kusahauliwa ya nyuma. Kujitangaza kushinda kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenyewe hakuelekei kujenga mazingira hayo.

Kwa mwelekeo huo, lengo la kujenga mazingira mapya ya kuaminiana katika uendeshaji wa siasa nchini linatoweka. Kauli za kutokubali matokeo ya kushindwa katika uchaguzi ujao zinajitokeza. Aidha, zinaonekana hisia za uchochezi wa uvurugaji wa amani na zinazotishia kutothaminiwa kwa makubaliano yaliyofikiwa kwenye muafaka huo.

Kuna haja ya kujenga mazingira mazuri ya kudumisha ustaarabu wa kisiasa wa kupingana bila ya kupigana na kushindana bila ya kuzozana ingefaa katika kipindi hiki cha uandikishaji. Viongozi wa vyama wawahamasishe wafuasi wao wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza kutumia haki yao hiyo bila ya kuwapandisha jazba za kurejea miaka ya nyuma.

Tamko la hivi karibuni lililotolewa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba chama chake kitafanya ‘mapinduzi yenye muundo wa Ukraine’ haliashirii kuendeleza msisitizo huo wa Muafaka zaidi ya kuwatia hofu wananchi na dunia kwa jumla.

Ubaya wa tamko hili ni kwamba limefanywa kwa kujificha. Kama ilivyo kawaida ya kiongozi huyo ya kutangaza mambo ya hatari anapokuwa nje ya nchi na kujifanya mwema awapo nchini, amelitoa tamko hilo alipokuwa akizindua kampeni ya chama chake huko Nairobi nchini Kenya.

Ni jambo la kushangaza kusikia kiongozi wa Tanzania anazindua kampeni zake za uchaguzi Kenya mahala ambako hakuna wapiga kura. Inaonekana kwamba kiongozi huyo alifanya hivyo kwa kutafuta kuungwa mkono lakini matokeo yake imezusha hofu, woga na wasiwasi.

Wasiwasi umewaingia watu wengi kiasi cha Ofisi ya Ubalozi wa Marekani nchini kuchukua hatua ya kutoa tahadhari kwa raia wa Marekani ili wasitembelee Zanzibar katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi huo kwa kuhofia kutokea ghasia na vurugu.

Chanzo cha tahadhari hiyo ni kauli ya kiongozi huyo anayegombea urais wa Zanzibar ambaye hapana wasiwasi wowote ameshabaini kushindwa kwake lakini bado anaonekana kutokubali matokeo yatakavyokuwa kwani ameshatamka kuyakataa hata kama atashinda.

Mara kadhaa, Katibu Mkuu wa CUF amekuwa akitoa matamshi yake ya vitisho kwamba nguvu ya umma itatumika kwa kuandaa maandamano kupinga kile anachodai uonevu unaofanywa na CCM na serikali zake kuhusiana na masuala ya uchaguzi.

Lakini kabla ya hata mzozo huo kuhusu idadi ya wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura haujatokea, tayari kulikuwepo na chokochoko kutoka chama hicho kuhusiana na uchaguzi mkuu huo.

Katika kipindi cha uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari hilo kulijitokeza matukio kadhaa ya kusikitisha huko Pemba ambapo miongoni mwa matukio hayo ni kumwagika kwa damu ambapo chimbuko lake lilitokana na baadhi ya wafuasi wa CUF kujaribu kujipima nguvu na vyombo vya dola.

Baadhi ya viongozi waandamizi wa CUF walikwishatamka wazi kuwa damu itamwagika wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka huu kwa kile wanachodai kuwa ikiwa wataibiwa tena kura kwenye uchaguzi mkuu.

Katika kutoa vitisho hivyo vya umwagaji damu, viongozi hao wa CUF wamekuwa wakikaririwa mara kwa mara wakisema kuwa watahakikisha kuwa mgogoro huo wa Zanzibar unasambaa nchi nzima na wala siyo Zanzibar peke yake.

Mbali ya vitisho hivyo, viongozi kadhaa wa CUF pia wamekuwa wakiendesha propaganda chafu dhidi ya CCM, ambapo wamekuwa wakiituhumu eti CCM ina vikundi vya mauaji vilivyobatizwa jina la ‘Janjaweed’ linalotumika huko Sudan katika kuendesha mauaji huko.

Kwa kuzingatia kauli za viongozi hao wa CUF, hali ya utulivu inaweza ikatiliwa mashaka. Kauli za viongozi hao, kimsingi, haziwezi kupuuzwa, kwani zinaweza kuchochea ghasia na kuitumbukiza Tanzania kwenye mgogoro wa kisiasa, fujo na ghasia.

Hisia hizo za kuibiwa kura zilianzishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho mwalimu Seif Sharif Hamad toka alipokuwa chama cha Mapinduzi. Mwaka 1985 ndani ya mfumo wa chama kimoja alidai kuibiwa kura, Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ilipomteua Mzee Idris Abdul Wakil kuwa mgombera urais wa Zanzibar na kumwacha Hamad. Kilio hicho cha kuibiwa kura kikitlewa tena katiak uchaguzi wa mwaka 1995 na 2000.

Lakini wakati tukitafakari jambo hilo kuna haja ya kufahamu sababu za kutokea vitisho vya aina hiyo. Sababu hasa ni wapinzani na Maalim Seif kutokubali kushindwa katika uchaguzi wowote wanaoshiriki.

Kauli za aina hii zinaonesha jinsi CUF kinavyojiandaa kutaka kuitia nchi katika misukosuko ya kisiasa na kusitisha kasi ya maendeleo ambapo Serikali itapaswa kujidhatiti vya kutosha kudhibiti hali hiyo.

Aidha, wananchi nao kutokubali kutishika kwa kauli hizo kwa kutowaunga mkono viongozi wenye kutoa kauli za vitisho. Hivyo, wananchi wasipoteze fursa ya kutumia haki yao ya kushiriki katika kuchagua viongozi wanaowapenda.


Mwisho.
DEMOKRASIA NINI!

DEMOKRASIA inamaana pana sana katika uwanja wa siasa. Asili ya neno Demokrasia linatokana na lugha ya Kiyunani (Kigiriki) ambalo msingi wake ni maneno mawili DEMO ambalo maana maanayake watu na KRATOS likiwa namaana ya uyo mtutawala. Kwa kifupi maana ya neno ni Utawala wa Watu, kwa kumaanisha matakwa ya watu wengi. Na kinyume chake ni Autokrasi ya Udikteta. Kwa ufupi Demokrasia maana yake ni wengi wape au kukubali na kuheshimu maamuzi ya wengi. Kwa maana hiyo mtu hawezi kuwa mwanasiasa, bila kuwa mwanademokrasia, lakini inawezekana kuwa mwanademokrasia pasi na kuwa mwanasiasa. Kwa kuwa demokrasia ndio msingi mkubwa wa siasa, hivyo mwanademokrasia anaweza kuwa mwanasiasa mzuri kwa sababu ana msingi madhubuti wa kuelekea kuwa mwanasiasa.

Hata hivyo, mtu anaweza akawa na sifa zote hizo mbili na pia inawezekana akawa hana sifa hata moja katika hizo, lakini akajipa sifa hizo kwa nguvu. Kwa kukamilika, mwanasiasa mzuri lazima awe pia mwanademokrasia.Mwanasiasa mzuri lazima awe mtu mtaratibu, mpole, mstaarabu na mwenye kushauriana na wenziwe na awe anakubali kukosolewa. Kubwa zaidi awe mwenye subira na mstahamilivu, kupungukiwa na sifa hizo, ni kukosa muhimili wa kuwa mwanasiasa.

Mwanasiasa siku zote huwa mkweli na muaminifu anayoyasema hayatofautiani na anayoyatenda Kwasababu hao waliojipachika uwanasiasa maneno yao tafauti kabisa na vitendo vyao, basi hatuwezi kuwaita wanasiasa bali ni wababaishaji tu wa siasa.

Nchini Tanzania tangu uanze mfumo wa vyama vingi, mwaka 1992 karibu kila mtu anajifanya mwanasiasa na wengine kudiriki kuunda vyama. Kwa kuangalia nyendo za watu hao inaonekana wanapenda kuwa wanasiasa bila ya kuwa na misingi ya uwanasiasa, hivyo wanashindwa hata kukaribia kufikia hadhi hiyo.

Katika kufuatilia kwa karibu nyenendo za baadhi ya wanasiasa, imebainika baadhi yao huwa wanatafuta kura za wananchi ili ziwawezeshe kutimiza matakwa yao ya kajipatia umaarufu, maslahi binafsi na katambulika ili waweze kupatamadaraka.

Kigezo nakipimo kikubwa cha kumfahamu mwanasiasa, kiko katika kuangalia nyendo zake na kuzilinganisha na misingi ya demokrasia. Misingi hiyo inazingatia Uhuru na Haki, kupinga aina zote za ubaguzi, ama wa rangi, kabila, dini, jinsia au umajimbo na kutoa haki yakila mtu kushiriki katika mambo ya utawalawa nchi. Jambo la muhimu katika misingi hiyo ni nidhamu, inayolazimisha wacheche wakubaliane na matakwa ya wengi,kila mtu awe na haki kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Kwa mtazamo huo demokrasia inaweza kuwapa mahali popote ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa au katika mfumo wa chama kimoja mradi tu, misingi hiyo mikubwa inafuatwa. Hivyo demokrasia nchini Tanzania ilianza tangu enzi ya mfumo wa chama kimoja.

Zanzibar imeshuhudia awamu tofauti za uongozi. Pamoja na yote hayo kumekuwa na baadhi ya watu wanadai ukombozi wanchi. Swali liliopo ni nani anayetawala Zanzibar! Jibu lake linaweza kuwa na utata, kwani litahusishwa moja kwa moja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imemezwa na Tanzania Bara. Kutakana na majibu ya aina hiyo ndipo hoja ya kusema kwamba kuna watu wanaojiita wasiasa, inapopata nguvu, kwani mwelekeo wa watu hao sio kujenga Taifa lenye nguvu, bali ni kudhofisha na kuleta mgawanyiko miongoni mwa jamii. wa Zanzibar katika kipindi hiki, wanataka kuikomboa Zanzibar kutoka katika mikono ya nani! Zanzibar hivi sasa inatawaliwa na wananchi wenyewe, wanyonge, wavuja jasho, wakwezi na wakulima. Anayetaka kuondoshwa madarakani ni nani! Na nani awekwe badala yake.

Nadharia hiyo ya kudai ukombozi ndani ya Taifa huru iliibuka katika kipindi kirefu ndani ya mfumo wa chama kimoja cha siasa. ASP na baadae mwaka 1977 CCM Mjaribio kadhaa yasiofaulu ya kutaka kuipindua Serikali ya Zanzibar yaligundulika moja kati ya hilo ni lile lililopelekea kuuwawa kwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume, Aprili 7, 1972. Mjumuiko wa matukio hayo, ni ishara iliyowazi kwamba athari za siasa za vyama vilivyokuwepo kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ziliendelea kubaki licha ya vyama hivyo vilivyokuwa vikipigania uhuru kuvunjwa baada ya Mapinduzi hayo. Hivyo wafuasi pamoja na baadhi ya vizazi vyao walikuwa wakiendesha sera za vyama hivyo za kugombania ukombozi.

Kikwazo kikubwa kilichosiisha kutimiza kwa azma hiyo ya wafuasi wa vyama vya kale ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao kwa muundo wake, siojambo linalowezekana kuipindua Serikali ya Zanzibar pekeyeke bila ya kuihusisha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla. Hivyo jmabo linalohitajika kufikisha lengo hilo ni kuparaganya muungano huo ambapo hila na mbinu mbali mbali za kuuvunja zilipangwa na kutekelezwa kufanikiwa.

Kuja kwa mfumo a vyama vingi nchini 1992 na kuanzishwa kwa chama cha upinzani Zanzibar hasa Chama Cha Wananchi (CUF), kuliipa nguvu mpya mikakati hiyo kwani mbinu zilizotumika katika kukisimamisha chama hicho, zilikuwa hazina tofauti na zile zizotumwa kuvisimamisha vyama vya zamani ZNP na ZPPP na hasa Pemba. Wananchi walishurutishwa kujiunga na chama hicho, na walionekaniwa kutounga mkono CUF,walitengwa, walisuswa kununuliwa bidhaa zao, waligomewa kuuziwa bidhaa kwenye maduka na masoko,walitengwa kwenye shughuli za kijamii kama vile misikitini, mazikoni maharusini makazini nk,walinyimwa hata maji ya kunywa visimani. Pamoja na shinikizo zote hizo wapo waliokataa kuiunga CUF, hao hao walifanyiwa vitendo vya kinyama kabisa, waling’olewa mazao yao katika mashamba, walihamishwa kwa nguvu katika mitaa, wanaume waliachishwa wake zao na kwa wanawake waliachwa na waume zao, na wengine kufika hata kupakiwa kinyesi cha binaadamu kwenye milango na
madirisha ya nyumba zao.

Harakati hizo zilianzishwa na kundi maalum ambalo hapana shaka lina malengo iliyo kusudia.Mipango hiyo inaweza kuhusishwa naile iliyokuwepo wakati wa kugombania uhuru. Lakini katika kufahamu kwa uwazi chimbuko la yote hayo, ipo haja ya kufahamu mwenendo wa muelekeo wa kiongozi mkuu wa kundi hilo kuanzia enzi za kudai uhuru, wakati wa mfumo wa chama kimoja na kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kiongozi huyo nikatibu Mkuu wa CUFMaalim Seif Shariff ambaye anatarajia tena kuwa mgombea wa Kiti cha Urais wa Zanzibar kwa mara ya tatu katika Uchaguzi mkuu ujao 2005.

KUJULIKANA KWA MAALIM SEIF
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye anategemea sana na wafuasi wake kuna haja kumtiza ma kama kweli ana sifa za mwanasiasa na mwanademokrasia wa kweli. Sief Shariff Hamad alianza kujulikana Zanzibar baada ya Mzee Aboud Jumbe Mwinyi kumteuwa kuwa Waziri wa Elimu mwaka 1977 na baada ya kuunganishwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM.

Maalim Seiff alikuwa mwalimu katika skuli ya Sayyid Abdalla ambayo hivi sasa inajulikana kwa jina la Fedel Castro, ambapo alikwenda kufundisha mara baada yakumaliza masomo yake ya kidatu cha sita katka Skuli King Geoge hivi sasa inajulikana kwa jina la Skuli ya Sekondari ya Lumumba. Alizaliwa Mtabwe katika kitongoji kinachoitwa Nyali, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, na kupata elimu yake ya msingi katika Skuli ya Uondwe na hatimaye kumaliza masomo yake ya elimu ya juu katika Skuli ya King Geoge. Mnamo mwisho wa miaka 1960 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi ya kuandaa Wataalamu na viongozi wa baadae, iliwapeleka wanafunzi wake nchi za nje kujifunza fani mbali mbali. Seiff, alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi hao waliopelekwa kwa ajili ya kuchukua taaluma katika vyuo vya nchi za nje.
Kwa wakati ule hao wote waliopelekwa nchi za nje walikuwa wanaandaliwa kuwa viongozi na makada watakaoshika nyadhifa mbali mbali za uongozi. Kwa sababu kipindi hicho hakikuwa kirefu tangu kufanyika Mapinduzi yaliyomuondoa Sultan, waliopatiwa nafasi hizo walilazimika waangaliwe kwa kuchunguzwa hasa misimamo yao kisiasa. Seiff katika kuchunguzwa itikadi yake ya kisiasa ikabainika alikuwa na msimamo wa ki-Hizbu tangu alipokuwa Beit-el-Ras. Akiwa bado mwanafunzi alianzisha Chama cha wazawa wa Pemba mapema mwaka1961, Chama hicho kilitumika kukiibia kura Chama cha ZNP (HIZBU) hasa katika Uchaguzi wa mwisho mwaka 1963. Hali hiyo iliwezekana kutokana na MaalimSeiff kuwa karibu sana na Zaim Ali Muhsin, Maulid Mshangama, Ibun Saleh, na Abduirahman Babu. Alishiriki mara nyingi katika mikutano ya siri ya ZNP iliyokuwa ikifanywa na Maulid Mshangama wakati huo alipewa tuzo ya kumuoa mtoto wa kifalme aitwae Amal. Walikuwa kila jioni walienda Beit-EL-Ras kufanya mazoezi ya kutembea ufukweni, huku kila siku Seiff akiwa ndiye aliyekuwa akiwatembeza. Akishirikiana na Ali Muhsi, Seiff aliwahi kuandaa Maulid I Beit-EI-Ras 1963 kwa njama ya kuwakutanisha pamoja Ali Muhsin na Mzee Karume, ambaye walimualika na akahudhuria. Baadaye Seiff alitangaza ASP imeungana na ZNP.Hivyo Chama cha Wazawa wa Pemba kilishiriki kikamilifu katika wizi wa kura wa kiti cha Darajani 1961. Wizi huo wa kura ndio uliokuwa sababu ba chimbuko hasa ia vita vya Juni. Mwak 1963 wakati ASP ilipojidhatiti kukichukua kiti cha Darajani kwa kumueka mgombea wake Mzee Thabit Kombo. Juma Ngwali kwa kushirikiana na chama cha Wazawa wa Pemba, chini ya uongozi wa Seiff walikabidhiwa meli ya Jamuhuri wakati huo ikiitwa Sayid Khalifa (jina la mmoja kati ya Wafalme waliotawala Zanzibar) kwanda kuchukuwa watu Pemba kwa ajili ya kupiga kura kwa Mgombea wa ZNP, na kiti hicho kilichukuliwa na ZNP. Seiff alisikika akijigamba kuwa juhudi zake zimeleta mafanikio. Kutokana na ushahidi huo, jina la Seiff liliondolewa katika orodha ya wanafunzi watakaokwenda kupata mafunzo ya nje yanchi liha ya kuwa alikuwa ameshafika Unguja kwa safari. Ilioekana kuwa sio busara kumrudisha tena Pemba, ndipo ilipoamuliwa apelekwe katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba akafundishe. Maalim Seiff Sharifu aliendelea na kazi ya kufuni disha mpaka mwaka 1972 baada ya kifo cha Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar ambapo nafasi yake ikashikiliwa na Bwana Aboud Jumbe. Katika kipindi cha utawala wake Jumbe, wakati huo Waziri wake wa Elimu akiwa Bwana Said Iddi Bavuai na Naibu Waziri Bwana Aboud Talib, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mara ya kwanza ilipeleka wanafunzi kumi na moja kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam. Waliteuliwa vijana hao waliofaulu vizuri masomo yao ya kidatu cha sita na kupelekwa Chuoni huko pamoja na vijana hao aliteuliwa na Seiff Sharif yeye akiwa Mwalimu katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba. Vijana hao ni -:
1. Abdalla Ismail Kanduru
2. Abubakar Khamis Bakari
3. Aziza Ali Saidi
4. Iddi Pandu Hassan
5. Juma Duni Haji
6. Mabrouk Jabu Makame
7. Mbarouk Omar
8. Moh’d Mwinyi Mzee
9. Omar Ramadhan Mapuri
10. Said Gharibu Bilali
11. Seiff Sharifu Hamadi

Kama kawaida katika kufanya hadhari ya kuteua vijana, Wizara ya Elimu ilikuwa na kazi kubwa ya kufanya uchaguzi juu ya misimamo yao kisiasa, jambo ambalo lilipelekea wajumbe wa Kamati aya Wizara kubishana, hatimae Mzee Jumbe akashauri kuw ani vizuri kusahau tofauti zilizokuwepo za kisiasa na waachiwe vijana wapate elimu ili kuja kulitumikia Taifa.
Wakiwa katika mazingira ya Chuo Kikuu, mawazo ya kutaka kuleta mabadiliko ya maendeleo Zanzibar yaliibuka na kuwatawala vijana hao. Hali ya kutoridhika na baadhi ya mwenendo na maamuzi yaliyokuwa yakichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibaryaliingia katika vichwa vya baadhi yao. Kutokana na hali hiyo, kulijengwa msimamo na vijana hao kwamba yeyote atakayebahatika kapata nafasi ya juu, ajitahidi kuwavuta wenzake ili wasaidiane katika maendeleo ya haraka.
Baada ya kumaliza masomoa yao, wakiwa wote wamechukuwa shahada ya kwanza ilioambatana na ualimu, isipokuwa watu watatu, Seiff Sharifu alichukuwa Shahada ya kwanza katika Social Science, Iddi Pandu na Abubakar Khamis wao walichukuwa Shahada ya Sheria. Baada ya kumaliza masomo yao walirejea Zanzibar. Naibu Waziri wa Elimu Bwana Aboud Talibu aliongozana nao hadi kwa Rais Jumbe kwa nia ya kumfahamisha kuwa vijana hao wamemeliza masomo yao na wako tayari kulitumikia Taifa. Rais Aboud Jumbe kwa sababu alimkumbusha Seiff Sharifu kwa kuwa aliwahi kumfundisha King Geoge kabla hajaacha kazi ya ualimu na kujiunga na siasa, aliagiza wale wahitimu kumi wapangiwe kazi na Seiff Sharifu akampa kazi Ikulu. Waliobaki mbali ya waliosomea sheria walipewa Chuo cha Ualimu Nkuruma kwa kazi ya kufundisha. Maalim Seiff alifanya kazi kwa uhodari mkubwa mpaka akafikia cheo cha Katibu wa Rais, hadi mpaka pale alipoteuliwa na Rais Jumbe kuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa maana hiyo aliyemfanya ajulikane Maalim Seiff Zanziba, na hatimae Tanzania nzima, ni Mzee Aboud Jumbe. Na alifanya hivyo kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano wa Wazanzibar.

AKIWA WAZIRA WA ELIMU
Mtu wa kwanza aliyebahatika kupata wadhifa mkubwa miongoni mwa vijan hao alikuwani Maalim Seiff alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu. Kwa kiasi Fulani alitekeleza ahadi waliopeana na wenzake kwani aliwavuta Mbarouk Omar na Omar Ramadhan Mapuri wakiwa ni watu wa karibu yake sana na kutokana na kufahamu kuwa anafanya kazi na wenzake Maalim Seiff alianza kujijengea ngome ya kufanya atakavyo kwa kuamini wasaidizi wake hawawezi kumsaliti kutokana na kuwa yeye ndiye aliyewapendekeza kuteuliwa kushika nafasi hizo.

Akiwa Waziri wa Elimu ndipo alipoanza kutekeleza sera za ubaguzi kuwagawa Wapemba na Waunguja . Kila kitu ikiwemo nafasi ya nyingi za mzsomo zilielekezwa Pemba na kuwapa zaidi jamaa zake hasa wa Mtambwe. Alifanya hivyo kwa kuelewa kuwa Serikali imeweka utaratibu mzima wa kuangslia mgao wa nafasi za masomo ya juu kwa sehemu ya Unguja iliokuwa na wakaazi wengi, kupatiwa nafasi sita na Pemba nne kwa kila nafasi 10 zilizopatikana Akiwa Waziri wa Elimu Zanzibar, Maalim Seiff alibadilisha mfumo huo na kuweka nafasi sita kwa Pemba na nne kwa Unguja, tena katika nafasi hizo nne za Unguja, hutafytwa wale wenye asili ya Pemba ambao wanaishi Unguja na kupatiwa nafasi hizo na kukifanya kisiwa cha Unguja kutopata nafasi hata moja.Alipobaini mpango wake huo huenda ungegunduliwa, alibuni mbinu nyengine ya kuwapeleka masomoni katika vyuo vya Bara vijana wa Pemba kwa kuwapeleka vyuoni moja kwa moja bila ya kuwapitisha Wizarani,na Serikali Muungano ilipouliza, Maalim Seiff kwa niaba ya Zanzibar alithibitisha kuwa wanafunzi hao waliteuliwa kihalali na SMZ. Na wengi kati ya wanafunzi waliopelekwa kwa mtindo huo walikuwa hawana sifa za kujiunga na vyuo hivyo. Aidha Maalim Seiff alidiriki kuwaondoa wafanyakazi wenye nyadhifa za juu katika Wizara wenye asili ya Unguja na kuwashusha vyeo na kuwapa jamaa zake wa Pemba. Hali ilipozidi kuwa mbaya na kuchukiza zaidi baada ya Maalim Seiff kuhusika pia na kashfa ya ubadhirifu wa fedha za mradi wa madawati ya Skuli. Ndipo Rais Aboud Jumbe aliparifiwa vlio vya muda mrefu vya wananchi waliokuwa wamechoshwa na vitendo vya upendeleo vilivyokuwa vikifanywa na Maalim Seiff. Rais Jumbe alichukuwa hatua ya kumuondoa katika wadhifa wake huo. Kuanzia siku hiyo Maalim Seiff alianza kujenga chuki dhidi ya Mzee Jumbe, kwa kudai kwamba amemuonea kufuatia kumuondoa katika wadhifa wake waWaziri wa Elimu.

HAMADI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Kutokana nawadhifa aliokuwa nao wa Waziri wa Elimu Maalim Seiff aliweza kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, aliitumia vyema nafasi hiyo kwa kuhakikisha kundi lake linaingia katika uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi akijua kuwa ndio nguzo pekee atakayoshikilia.Kwa kuwa Maalim Seiff wakati anafukuzwa Uwaziriwa Elimu, alikwishakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, aliitimia nafasi hiyo kujijenga zaidi na pia kumfitini Mzee Jumbe kwa Mwenyekiti wa CCM Mwalimu Julius K. Nyerere kuwa Mzee Jumbe kwa kushirikiana na waasisi wa ASP na Mapinduzi hawapendi wasomi. Hatimaye Mwalimu Nyerere aliishika fitna hiyo, jambo lilimpelekea Mwalimu kumchukua Maalim Seiff kumuhamisha Bara ambako alimpa kazi ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Hapo ndipo Maalim Seiff alipoitumia nafasi hiyo kujijenga kwa Mwenyekiti wa CCM, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwa kipenzi chake.

Akiwa Makao Makuu ya Chama huko Dodoma, ubaguzi aliokuwa nao na kuwapendelea jamaa zake aliendelea nao. Nafasi aliyopewa aliitimia kwa kuwapatia nafasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi watu wake kadhaa waliokuwa karibu naye. Kwa sabaubu Maalim Seiff ameshakamata mpini aliitumia nafasi hiyo kumfyeka yeyote ambaye alikuwa hakukubaliana na mawazo yake. Aidha aliendelea tabia ya chuki dhidi ya viongozi waasisi wa ASP, na kumpelekea kuwaona viongozi hao kuwa ni maadui na kuanzisha kuwaandama.

Maalim Seiff aliitumia vyema nafasi hii, na kufanya achaguliwe tena kuwa Mjumbe wa Kmati Kuu ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mapinduziuliofanyika mwaka 1982. Mwalimu Nyerere hakumshitukia mapema akampa wadhifa wa kuwa Katibu wa Halmashuri Kuu ya Taifa akiongoza Idara ya Uchumi katika Sekretarieti hiyo ya NEC. Akiwandani ya Sekretariet, Maalim Seiff alifanya kazi ya kuichimbai Serikali ya Zanzibar kwa kuendelea kumuandama Mzee Aboud Jumbe kwa kushirikiana na watu wake aliofanikiwa kuwapenyeza ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Wakati huo walikuwa wameshaunda kikundi cha siri walichokuwa wanakiita PEMBA LEBERATION ORGANAIZESHENI (PLO)uhudi ya Maalim Seif na wenzake zilifanikiwa kumuangusha Mzee Jumbe baada ya kujenga hoja kuwa Mzee Jumbe anataka kuvunja Muungano wa Tanzania. Walifanikiwa kwa siri kupata waraka wa mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyokuwa ywasilishwe mbele ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu muundo wa Muungano wa Serikali tatu. Maalim Seif na wenzake walidai kuwa Mzee Jumbe anataka Muungano wa Serkali tatu (3). Hii nathibitika pale waraka huo ulipowasilishwa na mmoja ya Mawaziri wa SMZ mbele ya Kamati Kuu Baadhi ya vijana wa Zanzibar wakiongozwa na Malim Maalim Seif walioshikilia kuondoshwa kukodishwa madarakani Mzee Jumbe. Wakati mmoja wa Mawaziri wake wa karibu alipokataa shauri hilo, walimuandama kwa kumwambia kuwa yeye ni kibaraka wa MMzee Jumbe na alifika hatua ya kutishiwa hata maisha yake kwa kuambiwa kuwa atauliwa. Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu mwenye asili ya Pemba aliasa kwa kuwambia wajumbe wenziwe wasiwe na haraka, kwani Mzee Jumbe kama binaadamu siku moja ataacha madaraka kwa njia moja au nyengine. Mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM, Maalim Seif na wenzake walimuadhiri Mzee Jumbe. Pamoja na madai ya kutaka kuvunja Muungano pia walifanikiwa kuwadanganya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka Bara, kuwa Mzee Jumbe alikuwa anataka kutumia “Revolution Justice” yaani hukumu za Kimapinduzi dhidi ya watu walioitwa wakorofi wa Zanzibar. Ukweli ni kuwa Mzee Jumbe alikwisha pata habari za kuundwa kwa (PLO) iliokuwaya wahusia wa kundi hilo walidhibitiwa ambao wengi wao walikuwa wakijiita kuwa ni waislamu wenye msimamo mkali.

Kutokana na kadhia hiyo, Mzee Jumbe alilazimika kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi wan chi. Ndipo alipoteuliwa bwana AliHassanMwinyi kuwa Rais w muda wa Zanzibar mwaka 1984.. Baada ya kuteuliwa Mzee Ali Hassan Mwinyi kushikilia nafasi hiyo, Mwalimu Nyerere kwa kumuamini Maalim Seif, alimuomba Mzee Ali Hassan Mwinyi amchuue Maalim Seif ili awe Waziri Kiongozi wake apate kumsaidia kutuliza hali ya hewa iliyochafuka Zanzibar. Maalim Seif alirejea Zanzibar bila ya kuzingatia kilichopelekea kufukuzwa kwake katika wadhifa wa Waziri wa Elimu.

Baada ya kuapishwa tu Maalim Seif Sharifukuwa Waziri Kiongozi, alijionesha wazi hali halisi aliyinayo.Kwani hapo ndipo alipodhihirisha kuwa yeye ni chuikatika ngozi ya kondoo, kwani alilihutubia Baraza la Wawakilishi, kwa kutoa Hutuba ambayo asili mia moja (100%) ilikuwa inadhihirisha unafiki wa kiongozi huyo kwa kulinganisha na vitendo vyake vya sasa. Sehemu ya kwanza ya Hutuba hiyo, ilichapishwa katika Gazeti la Ijumaa Machi 9, 1984. na sehemu ya pili ilifuata toleo la siku ya pili yake.
Jambo jengine alilolifanya Maalim Seif wakati akiwa Waziri Kiongozi ilikuwa ni kuwaachilia waliodhibitiwa kwa kuhusika kwao na madai ya uhaini. Vijana hao walioachiliwa hivi sasa ni watu wake wa karibu katika shughuli za kisiasa.

Mzee Mwinyi katika kipindi chake kifupi akiwa na Maalim Seif alimstahamilia mambo mengi kwa sababu alijifanya kama yeye ndiye Rais wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kupendekeza kuwekwa Wakuu wa Mikoa wa Wilaya pamoja na vikosi vya Ulinzi vya (SMZ) watu kutoka Pemba ambako katika uendelezaji wwa mipango yake ya ubaguzi kati ya wazaliwa wa Unguja na Pemba. Kwa tabia yake hiyo ndio maaana maamuzi yote yalikuwa yakitolewa na Serikali alijifanya yanatokana na yeye.

Mara kadhaa amekuwa akijigamba kuwa yeye ndiye aliyeanzisha utaratibu wa ulegezaji wa masharti ya biashara Zanzibar. Ilionekaana hivyo ingawa ukweli ni kuwa mara baada ya kushuka kwa kiasi kikubwa Uchumi wa Zanzibarkutokana na kuanguka kwa bei ya zao la karafuu mwanzoni mwa miaka ya 1980, Mzee Jumbe ndiye aliyepeleka kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi mpango wa ulegezaji masharti ya biashara ili kuinusura Zanzibar na hali ngumu ya Uchumi. Hadi Mzee Jumbe anajiuzulu, mpango huo ulikuwa umeshapitishwa na NEC bado utekelezaji wake ambapo Mzee Mwinyi alipoingia madarakani aliukuta uko juu ya meza na kuanza kuutekeleza.

Hata hivyo Maalim Seif alijitangazia mpango huo ameubuni yeye. Aidha alijitangazia kuwa msaada wa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Gombani umetokana nay eye ingawa aliyekwenda Jamhuri ya Watu wa Korea kuomba msaada huo alikuwa ni Mzee Mwinyi.

Tabia hiyo ya kujitapa imechangia kuengea kasi ya kunawiri kwa mtengano wa Ki-kabila na Umajombo wa Upemba na Unguja, na ukazidi kupamba moto kwani Wapemba waliamini kuwa haya yote yameletwa na jamaa yao.

Akiwa Waziri Kiongozi alikuwa akipita katika ofisis za Serikali na pindi akibaini kiongozi katika sehemu hiyo bado hajafika zaidi akihakikisha kwamba nafasi hiyo inashikiliwa na mtu wa Unguja, alikuwa akimtimua na badala yake kumweka jamaa yake. Unyanyasaji kwa watu wa upande mmoja wa Zanzibar ulizidi sana. Mfano ulio hai inadhihirisha kuimarika kwa ubaguzi ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kwamba Maalim Seif alikuwa hana nafasi ya kukutana na mtu wa Unguja wakati jamaa zake walikuwa hawatoki ofisini na nyumbani kwake.

Chini ya usimsmizi wake alshiriki kuwanyang’anya magari yao na vitu vyengine wafanyakazi wa Meli ya M.V. Mapinduzi waliyoyanunua baada ya kujinyima wakati walipokuwa Japan ambako meli hiyo ilikwenda kufanyiwa matengenezo. Aliweza kulitekeleza hilo akijua kuwa kati ya wamiliki wa magari hayo hakuna jamaa yake.
Kwa kuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati huo akiwa Rais wa Zanzibar, alikuwa akisisitiza kuwa “Zanzibar ni njema atakae aje” Maalim Seif aliitumia nafasi ile kuwarejesha wale wote waliotamani kurudi Zanzibar ambao walikimbia baada ya Mapinduzi ya 1964.
Wengine alidiriki hata kuwarudishia baadhi ya mali zao zilizotaifishwa kisheria baada ya Mapinduzi ya Januari, 12.1964 ikiwa ni pamoja na kuwarejeshea nyumba zao watu waliorudi Zanzibar. Alitamani kuwarejashea wenyewe hata yale mashamba yalichukuliwa na Serikali, na kuwagaiya wananchi Eka tatu tatu. Katika kuendeleza mpango wake, Maalim Seif aliiandaa Waraka ambao aliuwasilisha kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya taifa ya Chama Cha Mapinduzi unaoeleza dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwanyang’anya wale wote waliopewa mashamba hayo baada ya Mapinduzi na ambao wanashindwa kuyaendeleza, na kugawiwa kwa wale wenye uwezo wa kuyaendeleza.Hapa Maalim Seif aliweka mtego na kama angelifanikiwa nia yake ilikuwa ni kuwanyang’anya wananchi eka tatu zao za ardhi walizopewa na Serikali ili ardhi hiyo wrejeshewe Mabepari waliokuwa wakihodhi kabla ya Mapinduzi ya januari, 12.1924. Alifanya hivyo akijua kuwa kunatofauti ya uwelewa kati ya wananchi wa Tanzania Bara na wa Zanzibar juu ya dhana ya mashamba. Kwani kwa Tanzania Bara, mashamba huwa hata yale ya anayolimwa mahindi na viazi ambayo hayana mazao ya kudumu. Hivyo baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambao walikuwa wajumbe wa kikao hicho wakamueleza Mwalimu Nyerere kuwa mashamba yaliyokusudiwa katikawaraka husika ni eka tatu walizopewa wananchi na Serikali baada ya Mapinduzi, wala si mashamba ya mahindi, maharage na viazi. Mashamba hayo yana miti ya kudumu na kati ya miti ya hiyo mengine imepandwa na wenyewe wananchi waliopewa ardhi hiyo. Aidha wengine kati ya wananchi hao wamejenga nyumba zao na wanaishi humo na familia zao. Kwa hoja hizo waraka huo ulikataliwa. Lengo la Maalim Seif lilikuwa ni kuwanyanga,nya ardhi wananchi wanyonge wa Zanzibar.

Maalim Seif alikwepa kuupeleka waraka huo kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi akijua fika ndani ya kikao hicho baadhi ya wajumbe wangegundua mpango wake na wasingekubali. Matokeo Mwalimu Nyerere akatoa uamuzi kuwa ardhi iliyogawiwa wananchi mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 iachwe kama ilivyo.

HAMADI KUSHINDWA URAIS WA ZANZIBAR KWA MARAYA KWANZA 1985
Kama ilivyo katika Katiba ya Zanzibar wakati Rais wa Zanzibar akiondoka madarakani kwa njia yoyote ile, atateuliwa zanzibari mwengine kushikilia wadhifa ho kwa muda wa siku tisiini, na wakati huo Uchaguzi wa Rais utaitishwa ili apatikane Rais aliyechaguliwa na wananchi ili amalizie kipindi kilichobaki. Wakati Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ilipokaa kupendekeza jina la Mgombea Urais wa Zanzibar,kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Kamati Kuu inateua majina ya wazanzibari wawili kupeleka kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa, na kupigiwa kura. Mshindi katika watu hao wawili ndie atakaekuwa mgombea aliyeteuliwa na Chama kwenda kupigiwa kura na wananchi. Kwa kuwa wakati ule Mzee Mwinyi ndiye aliyekuwa anashikilia kiti cha Urais wa Zanzibar, hivyo jina lake lilikuwa la kwanza kuzingatiwa. Kamati Kuu imependekeza mzanzibari mwengine ili kukamilisha majina mawili nae ni Mzee Idrisa Abdulwakil, wakati huo akiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mzee Idrisa alifanya kitendo cha kiungwana kilichowapelekea watanzania wotngaa, kwani Mzee Idrisa aliondosha jina lake katika kuwania nafasi ile na kumwache kushangaa, kwani Mzee Idrisa aliondosha jina lake katika kuwania ile na kumwachia MzeeMwinyi kupita bila ya kupingwa. Chama kikamteua Mzee Mwinyi kuwa Mgombea nafasi ys Urais wa Zanzibar, Uchaguzi ukafanyika na Mgombea huyo alichaguliwa kwa kura nyingi Unguja na Pemba.

Katika uchaguzi mkuu wa mwka 1985 baada ya Mzee Mwinyi kupendekezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nafasi ya mgombea Urais wa Zanzibar ilikuwa wazi. Hivyo ikabidi Chama kitafute mgombea mwengine. Kamati Kuu katika kipindi hiki ilimpendekeza tena Mzee Idrisa. Kwa hivyo jina la Mzee Idrisa likawa la kwanza, na kazi ikawa kutafuta jina la Mzanzibari wa pili. Kama kawaida yake Hamadi jinsi anavyopenda madaraka, na kwa kuwa nafasi hiyo alikuwa akiinyemelea kwa muda mrefu, kwa vile alikuwemo ndani ya Kamati Kuu. Aliitumia nafasi pale Mwalimu Nyerere ambae alikuwa ndie Mweyekiti wa Kikao alipotania kwa kusema “ Nani atamshindikiza Mzee? Hapo aliinuka Maalim Seif bila ya aibu na kusema “Mie´ Na kikao kikaunga mkono kwa kupiga makofi huku wajumbe wakidhani kuwa Hamadi ni muungwana kama alivyo mzee Idrisa. Kujipendekeza kwake kungekuwa na lengo la kuondosha jina kama alivyofanya Mzee Idrisa wakati alipokuwa yeye na Mzee Ali Hassan Mwinyi, ili kukiepusha Chama kuwa mgawanyiko kutokana na jambo hili. Hapo Kamati Kuu ikatoka na majina mawili la Mzee Idrisa Abdulwakil na Maalim Seif Sharrif Hamad, ambayo yalipelekwa kwenye kikao Halmashauri Kuu, kwa kupigiwa kura na mshindi atakuwa ndie mteule wa Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Rais wa Zanzibar. Inasemekana kuna kijana mmoja miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa alimtania Seif, na kumuuliza. “Eti nasikia umeamua kumshindikiza Mzee?” Maalim Seif alijibu. “Kumshindikiza maana yake nini? Mimi nagombea”. Kauli hii ya Seif ikawafanya baadhi ya vijan wenye uchungu na nchi kufanya kazi ya ziada kumfanyia Kampeni Mzee Idrisa. Na Seif nae na kundi lake kwa uapande wake wakakazana kufanya Kampeni ili kuhakikisha mtu wao anashinda nafasi hio. Kampeni zilikuwa ngumu sana, kwani kundi la Seif Shariff lilijidhatiti kufanya Kampeni za kumpaka matope Mzee Idrisa hasa mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu kutoka Mikoa ya Tanzania Bara. Miongoni mwa Kampeni yao kubwa ni kuwa huyu ndie miongoni mwa wazee wa Zanzibar wasiopenda mabadilikko na wasiowapenda wasomi. Na kwa upande wa vijana wanamapinduzi wa Zanzibar wakakaza kamba ya kuhakikisha Mzee wao anafanikiwa kwani wakijua kuwa nafasi hio pindipoikiingia kwenye mikono ya mpinga Mapinduzi, Mapinduzi yao yatakuwa hatarini. Wakati wajumbe wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano, karatasi za kupigia kura zimeshaandaliwa, katika kutawanya kuratasi hizo zenye maelezo binafsi ya wagombea, ambazo ziligunduliwa na kasoro katika kuziandaa. Kasoro hizo ni kuwa mgombea Seif Shariff kuwa na maelezo marefu yanayoelezea sifa zake, wakati Mzee Idrisa alipewa nafasi ndogo ya maelezo binafsi. Sifa na nyadhifa nyingi alizowahi kushika ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mara baada ya Mapinduzi, na Serikali ya Jamhri ya Muungano baada ya kuzaliwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hazikuelezwa. Hata lile tukio kubwa alilolifanya la kuacha kazi ya ualimu kwa hiyari yake, na kujiunga katika kundi la wapigania Uhuru kwa upande wa ASP nalo pia halikuelezwa. Vijana ndipo walipomwendea Mzee wao bwana Thabit Kombo kumueleza juu ya njama ile ilioandaliwa na Seif Shariff kupitia watu wake aliowapandikiza kwenye Chama kwa. Hivyo baada tu, ya kuanza kikao kijana mmoja alijichomoza kutoa taarifa mbele ya kikao juu ya kasoro hiyo. Na baadaa ya taarifa hiyo Mzee Thabit Kombo alinon’gona na Mwenyekiti wa kikao. Mwenyekiti alilazimika kukiakhirisha kikao kwa muda ili kusawazisha kasoro zilizojitokeza. Mwenyekiti aaliagiza kasoro zilojitokeza zisawazishwe na wagombea wote wawepo kwenye kikao, na kila mmoja apewe nafasi ya kujieleza mwenyewe.

Baada ya kupigwa kura na kuhesabiwa, Mzee Idrisa alimshinda Maalim Seif kwa kura 7, na alitangazwa na CCM kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1985. Kwa kuwa Maalim Seif alishindwa kuheshimu matokeo yale na kuanza kudai kuwa, amenyang’anywa nafasi yake ya kugombea urais wa Zanzibar, na hakupewa nafasi hiyo kwa sababu yeye ni Mpemba. Alieleza bayana kwamba alishinda lakini ameibiwa kura, na alisingizia kuwa Demokrasia na haki haikutendeka katika uchaguzi na kusingizia mambo kadhaa.

Kitendo hicho kilimjengea sifa mbaya na kuonekana kuwa ni kiongozi mwenye tabia mbaya ya ubinafsi na chuki na hasa alipoanza kujenga chuki kwa vijana wote aliowadhani kuwa hawakumuunga mkono.

Mwalimu Nyerere alibaini kuumia kwa Maalim Seif kutokana na kuikosa nafasi hiyo, hivyo alijaribu bila mafanikio kumpoza mpoyo kwa kumtaka awe na subira, na kumsisitiza aende Zanzibar kumpigia kampeni Mzee Idris, ili kuhakikisha anachaguliwa kwa kura nyingi.

Hata hivyo, Maalim Seif hakuzingatia ushauri na maelekezo aliyopewa na MwalimuNyerere. Alichokifanya Maalim Seif badala yakr ni kukusanya nguvu za kundi lake lililokuwa likimuunga mkono, muja Zanzibar kupiga kampeni dhidi ya maamuzi ya Chama. Alijidhatiti kuhakikisha Mzee Idris hachaguliwi kuwa Rais wa Zanzibar.

Wakati w harakati za kampeni Maalim Seif na wenzake, wengi wao wakiwa ni wazaliwa kutoka Pemba, walielekeza nguvu zao Pemba na kuhakikisha Mzee Idrisa hachaguliwi. Wananchi na hasa wa Pemba, walitiwa maneno ya fitna na kutakiwa wasimpigie kura Mzee Idris kwa kudai kuwa nafasi ya Urais wa Zanzibar safari hyo ni zamu ya watu wa Pemba, ila watu wa Unguja wanang’ng’ania tu kwa sababu wanawachukia wapemba. Iliendelezwa kampeni kwamba katika uchaguzi wa kutafuta Mgombea uliofanywa ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Maalim Seif ndiye aliyeshinda, lakini amedhulumiwa kwa kuibiwa kura.

Aliwaambia watu wa Pemba wasimchague Mzee Idris kwa sababu anawachukia wapemba, pindipo wakimchagua kuwa Rais wa Zanzibar atawaadhibu wapemba. Wpiga kura walishawishiwa kwa kuambiwa kuwa, kwenye karatasi ya kupigia kura pale palipo kuwa na ukuta nyuma yake kuna picha ya MaalimSeif, hivyo watakaopiga kura zao kwenye Ukuta watakuwa wamemchagua Maalim Seif. Maalim Seif alifanya hivyo kwa kuamini kuwa pidipo wananchi watakapo piga kura zao kwenye ukuta, na ikiwa Mzee Idriss atashindwa kupata kura za kumuwezesha kuchaguliwa, kwa mujibu wa katiba ya Chama italazimika vikao vya chama kukaa tena na kufikiria jina la mwanachama mwengine ili agombee nafasi hiyo. Na kwa fikra zake aliamini kuwa lingefikiriwa tena jina lake.

Maalim Seif na kundi lake waligawana kazi hiyo wengine Unguja kwa mbinu zao na wale wa Pemba wakiongozwa nay eye mwenyewe. Na kwasababu Maalim Seif ni mpemba na alikwisha wajaza kasumba wapemba wenziwe, kuwa wasimchgue Mzee Idris, matokeo ya Uchaguzi ule yalikuwa mabaya sana kwa Pemba, tofauti na hali ilivyokuwa Unguja. Matokeo mabaya ya Pemba hayakuathiri ushindi wa Mzee Idris kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar mwaka 1985. Hapa nataka kueleza kitu kimoja. Seif alipoelekea Pemba na kutia fitina kuwa ameonewa na kura zake zimeibiwa. “Siku zote mwizi hudhani watu wote ni wezi kama yeye. Na dhalimu siku zote hudhani kuwa watu wote ni Madhalimu kama yeye.” Lakini pamoja na njama zote hizo, hatimae Mzee Idriss alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Pamoja na matukio yote hayo, Mzee Idris baada ya kuchaguliwa alimteuwa tena Maalim Seif kuwa Waziri Kiongozi. Rais Idriss alimpa Seif haki zake zote, ikiwa ni pamoja na kumshauri katika kuunda Baraza la Mawazir. Maalim Seif aliitumia nafasi hiyo kama kawaida yake kupandikiza watu ambao wangetenda vyo vyote vile atakavyo yeye.

Kwa kuwa mambo aliyoyafanya Maalim Seif kwa kushirikiana na kundi lake haya kuwa siri, na yalikuwa kinyume na maadili ya CCM viongozi wa CCM wa Zanzibar walilijadili jambo hilo kataka vikao mbalimbali hadi kufikia katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika mara baada ya Uchaguzi huo, kwa kufany tathmini ya matokeo ya uchaguzi. Katika kulijadidi jambo hilo moja kwa moja Maalim Seif na kundi lake walionekana kuwa na makosa.

Lakini aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mwalimu J.K. Nyerere akitumainia kuwa Seif Shariff aliyafanya yale kutokana na joto la Uchaguzi tu, alikiomba kikao kimsamehe huku akidhani kuwa Seif Shariff atajirekebisha na kumapa ushirikiano wa kutosha Mzee Idris hasa kwa kuzingatia kuwa amekosa Urais lakini amepata Uwaziri Kiongozi.

Pamoja na kuwa Mwalimu Nyere, alishauri jambo hilo liachiliwe mbali, lakini mambo hayakuwa kama yalivyotarajiwa. Matokeo yake Seif Shariff na kundi lake walikuwa kama samba aliyewahi kula nyama ya mtu. Hawasikii wala hawaoni, akili zao zote zililenga kwenye nafasi ya Urais tu. Walianza kufanya vituko vya nuni Firauni. Kwanza walifanya kila mbinu ili kuhakikisha Mzee Idris inashindwa kuitawala Zanzibar. Walijipanga katika kila nafasi nyeti za kuongoza nchi. Kuanzia Uwaziri, Ukuu wa Mkoa Ukatibu Mkuu, Ukurugenzi, Umeneja hadi uafisa wa Serikali katika Wizara na Taasisi zake.

Walimsokota Mzee Idris asipate pumzi. Baraza la Mawaziri lilikuwa limegawika sehemu mbili, moja iliyomuunga mkono Rais na ya pili iliyomuunga mkono Waziri Kiongozi. Barazala Wawakilishi nalo halikadhalika. Kulikuwa na Wawakilishi wa Rais na wa Waziri Kiongozi. Hata chama cha Mapinduzi upande wa Zanzibar nacho kiligawika sehemu mbili, kulikuwa na viongozi na watendaji waliomuunga mkono Mzee Idris na vile vile walikuwapo wengine waliomuunga mkono Seif Sharuff. Kwa jumla hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar ilichafuka.

Seif Shariff alihakikiha kwamba anamjengea uadui Mzee Idrisa hata kwa wale wananchi anaowateua kuwapa dhamana mbali mbali ndani ya Serikali yake. Maalim Seif aliijenga tabia ya kujionesha mwema kwa kila mtu mbaye Rais alikuwa anataka kumkabidhi dhamana ya uongozi au utendaji katika Seriksli.

Silaha kubwa aliyokuwa akiitumainia, ni kuwaelezea watu hao yeye amewapendekeza kushika nafasi za uongozi na utendaji fulani, lakini Mzee Idris hataki. Alikuwa akiwauliza. “Jee, mmekosa nini Mzee? Bila shaka jawabu itakayopatikana hapo ni kushangaa. Kwa sababu pengine baadhi ya wananchi hao hata hawajawahi kukutana na Rais mwenyewe. Hapo Seif huendeleza fitna zake kwa kuwambia watulie kuwa atahakikisha wanateuliwa hata kama Rais hapendi.

Tabia hii iliwafanya wafuasi wa Seif kuamini kuwa yeye ndiye Rais, walifikia hatua ya kubadiliisha jina la tatu la Rais ‘NOMBE” na kuliita “NG’OMBE” huku wakishadidia kwa kusema “Ngo’ombe sasa anamfuata mchungawe.” Yaani Mzee Idrisa anamfuata Seif Shariff kwa kila alitakalo. Kadhia hii ilimpelekea washauri wa serikali kumshauri kuacha kutumia jina hilo la tatu kwa maudhi na karaha aliyokuwa akifanyiwa.

Lengo la Seif Shariff na kundi lake lilikuwa ni kuhakikisha kila aliyekabidhiwa madaraka ndani ya Serikali anaunga mkono kundi lao.

Maalim Seif na kundi lake walichukua ahadi kwamba watawaangamiza waasisi wote wa ASP. Katika kutekeleza azma hiyo, lilianza kwa kuandaa njama za kumuhusisha aliyekuwa Waziri wa kilimo bwana Hassan Nassor Moyo na Naibu wake bwana Abdulla Rashid na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa Makurunge. Hoja hiyo iliwasilishwa kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi na kundi hilo. Ukumbi ulikuwa moto, kwani baadhi ya wajumbe walisimama kidete kuwatetea bwana Hassan Nassor Moyo na bwana Abdulla Rashid. Kwa sababu walikuwa wanatetea msimamo wa kisiasa dhidi ya siasa za upinzani zilizojengeka ndani ya fumo wa Chama kimoja cha siasa, siri zilizokuwa hazifahamiki na wengi za Seif Shariff na jamaa ziiibuka. Hivyo Seif Shariff aliona mambo huenda yakaharibika, kwa kutumia wadhifa alikuwa nao wa Waziri Kiongozi haraka akaituliza hali hiyo ili kuepuka kuyaweka mambo yao hadharani.



Katika mtizamo wa suala la kuendeleza sera za Chama, Hamad licha ya kukabidhiwa Idara ya Uchumi ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM lakini alikuwa akiendesha mambo yake kinyume na maelekezo ya sera hizo. Kutokana na tabia hiyo ya kuwa ndumila kuwili akiwa na nafasi ya Uwaziri Kiongoziii alikwaruzana na Marehemu Jamal Ramadhani Nassibu kuhusu waraka ulikuwa na kurasa 25 unaoelezea historia ya ukombozi wa Mzanzibar.

Waraka huo uloandikwa na mzee Jamal Ramadhani Nasibu, na kuwasilishwa katika Semina ya Halmashauri Kuu za CCM Mkoa wa Mjini na Magharibi na Wilaya zake wakati huo Mzee Jamal akiwa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Kilichoonekana wazi ni kwamba katika kutekeleza majukumu yake kama Waziri Kiongozi Seif Shariff hakujali kazi alizokabidhiwa na nchi, bali aliitumia nafasi hiyo kujitafutia nafasi kubwa zaidi. Hakupenda kukaliwa na mtu juu yake. Ndio maana akatumia juhudi na uhodari wake wote kujitafutia Urais kwa njia yoyote ile. Seif na kundi lake waliendesha ufisadi katika nchi.

Seif alifanya kila aliloweza kuhakikisha Zanzibar haiendi mbele. Mali za serikali anazigawa kwa jamaa zake bila ya kujali kuwa ile ilikuwa ni mali ya wananchi. Aliandaa utaratibu uliyohakikisha nyumba za Serikali wanauziwa jamaa zake kwa bei sawa sawa na bure. Mali za Serikali ziliuzwa kwa bei ndogo zisizolingana na thamani ya mali zenyewe. Alitoa viwanja kiholela tu, mashamba ya Serikali yalitolewa kwa jamaa zake na pesa za Serikali zilikopeshwa kwa jamaazake bila hata kufuata taratibu na sheria za mikopo. Mashirika na miradi mbalimbali ya Serikali yalikabidhiwa watu ambao waliyahujumu bila ya hata kujali. Mfano hai ni kukabidhiwa kukiongoza kiwanda cha Maziwa kiliopo Maruhubi mtoto wa dada yake nae alifanya ubadhirifu wa hali ya juu jambo lililopelekea shamba la Ngo,mbe pamoja nakiwanda hicho kuangamia.

Baad ya baadhi ya viongozi walipoona nchi inaelekezwa siko ndipo walipochukua hatua ya kutoa taarifa kwenye vikao vya Chama kuanzia ngazi za chini na hatimaye kufikia kwenye Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi. Na matokeo yake mnamo mwaka 1987 wakati Halmashauri Kuu ya Taifa ya C.C.M. (NEC) ilipokaa katika kikaoo cha kujadili majina ya wana CCM walioomba uongozi katika ngazi za Wilaya, Mikoa hadi Taifa. Taarifa hizo ziliweza kusaidia na kupekea baadhi ya waomba uongozi wa ngazi hizo kutoka Zanzibar kutokuteuliwa kugombea nafasi hizo. Miongoni mwa hao ni:-

Ali Haji Pandu
Shaaban Khamisi Mloo
Khatibu Hassan na
Suleiman Seif Hamadi

Seif Shariff alisalimika kwa sababu ya heshima ya ujumbe wa Kamati Kuu, na nafasi aliyokuwa nayo ya Uwaziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini nae hatima yake ilimalizika kwa kukosa nafasi ya kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Maalim Seif alidhamiria hasa kuendeleza upinzani akiwa ndani ya Serikali na ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Baada ya kufanikiwak kuwateka viongozi na watendaji wa Chama na Serikali na kutokana na uchungu wa kuikosa nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ndipoalipoamua kupinda mgongo kwa juhudi na maarifa kuhakikisha azma yake ya kuparaganya nchi inafanikiwa. Ndipo baada ya kumaliza harakati za Uchaguzi Mkuu wa Chama wa mwaka 1987 Maalim Seif aliomba ruhusa ya kwenda Matibabuni Ulaya na Rais Idrisa akamruhusu, kumbe huku nyuma tayari chungu kinachochewa moto unarindima nacho kinatokota. Aliwaandaa baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Wkuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya, na kuwataka wamuandalie mapokezi makubwa nay a aina yake.

Mapokezi ambayo hajapata kupokelewa kiongozi yeyote hapa Zanzibar. Waliyaandaa mapokezi hayo kwa makusudi wakaamua kuwa yafanyike Pemba. Maalim Seif alirejea na alikaa Unguja kwa siku mbili tatu na mambo yalipokuwa tayari alikwenda Pemba, huku akimuaga Rais Idrisa kuwa anakwenda kupumzika. Alipofika Uwanja wa Ndege wa Karume Chake Chake Pemba Maalim Seif alilikuta alilolitarajia kwani kulikuwa na ummati mkubwa mno ambao ulikuwa unamngojea na kumpokea. Wengi wa watu hao hawakuwa wakijua nini kinachoendelea, kwani wao waliona kuwa Waziri Kiongozi wao amerejea kutoka matibabuni wanampokea. Baada ya kuteremka kwenye ndege na kusalimiana na viongozi na kutoka nje ya uwanja, palikuwa na Sheikh tayari ameandaliwa na hapo hapo ikasaliwa sala Maalum ya RAKAA mbili ili kumuombea dua Maalim Seif na kumuondoshea “DAFA-EL-BALAA”.
Kwa wale waliokuwepo siku hiyo wanasema Sheikh aliyeteuliwa kuomba dua baada ya sala ya rakaa mbili, aliomba dua kwa kusema: “Kama kiongozi huyu ana kheri na sisi basi Mwenyezimungu tuekee , la kama kiongozi huyu hana kherti na sisi basi utuondoshee”. Baada ya kumaliza dua hiyo, msafara wa miguu ulianza kuelekea mjini Chake Chake kwa maandamano, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Chama wa Mikoa na Wilaya pamoja na mwenyewe Maalim Seif wakiongoza maandamano hayo. Nyimbo zilizokuwa zikiimbwa katika maandamano hayo zilikuwa ni za matusi na kashfahasa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar pamoja na watu wenye asili ya Bara. Maneno ya nyimbo hizo yalikuwa Hatuyataki machogo; hatumtaki ng’ombe; hatuutaki Muungano; n.k.

Pamoja na hayo, Maalim Seif alidiriki kumfanyi kitendo kikubwa Mzee Idris kilichodhihirisha dharau, utovu wa nidhamu na udhalilishaji. Kwani wakati wa kipindi chake cha Urais Mzee Idris alipanga kwenda kufanya Ziara Pemba, aliondoka Unguja yeye na msafara wake kwa kutumia usafiri wa ndege hadi Pemba. Alipofika Pemba aliikuta Ikulu imefungwa kwa kufuli, na wakati huo Ikulu ilikuwa ikiiangaliwa na kutunzwa na Mkuu wa Mkoa. Aliyekuwa akishikilia nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba wakati huo alikuwa ni Maalim Juma Ngwali Kombo, mtu aliyepandikizwa na Maalim Seif kwa madhumuni niliyokwisha kuyataja huko nyuma.

Maalim Seif alimuamrisha Mkuu wa Mkoa afunge Ikulu na aondoke pamoja na funguo zote, kwani hakupenda Rais Idris aende kufanya kazi za nchi katika kisiwa cha Pemba. Jambo ambalo lilimpelekea Mzee Idris kupata usumbufu mkubwa na hatimaye aliamua kurudi Unguja bila ya kufanya kazi alizozikusudi. Jambo hili lilimsikitisha sana Mzee Idris, na kusikika akisma hadharani. “Huyu Seif anataka nini? Kama ni urais si asubiri, mimi bado miaka miwili tu, nimalize muda wangu. Nikimaliza kipindi hiki tu ninamuachia yeye. Hiyo ilikuwa mwaka 1998.

Kutokana na matukio niliyoyataja na mengi menginyo yaliyofanywa na Seif Shariff na kundi lake huko nyuma, Chama cha Mapinduzi kwa makusudi kiliamua kuwaleta baadhi ya Watendaji wa Wilaya na Mikoa kutoka Tanzania Bara kuja kufanya kazi za Chama katika Mikoa na Wilaya za Zanzibar.

Watendaji hao waliotoka Bara kuja kufanya kazi za Chama Zanzibar walishuhudia kwa macho yao matendo ya kuvuruga Umoja na Mshikamano wa Chama cha Mapinduzi hapa Zanzibar vilivyokuwa vinafanywa na Maalim Seif akishirikiana na wafuasi wake.

Mzee Idriss, baada ya kuchoshwa na vitendo vya Seif Shariff na wafuasi wake ndipo alipoamua kulivunja Baraza la Mawaziri na kuliunda upya. Katika hatua hiyo aliyoichukua Seif Shariff alimfukuza Uwaziri Kiongozi, lakini wale Mawaziri wengine wote aliwarudisha kwenye nafasi zao za Uwaziri. Rais Idris alimteua Dr. Omar Ali Juma kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ badala ya Seif Shariff Hamad. Hapo Mzee Idris alikuwa kama aliyeongeza Petrol katika moto unaowaka. Wafuasi na wapenzi wa Seif Shariff wakadai kuwa Mzee Idris amemuonea Maalim Seif, amemnyang’anya Uwaziri Kiongozi wake. Alimuradi Nchi iliingiwa na mtafaruku. Lakini kutokana na hekima na Busara za Mzee Idris aliweza kuiongoza nchi kwa makini sana.

Kutokana na yote hayo yaliyokwisha kuelezwa imeonesha dhahiri kwamba Maalim Seif alikuwa mpinzani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu ASP na hatimae CCM, aidha hakuwa muumini wa kweli wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ingawa katika kauli zake mbali mbali wakati akiwa madarakani alisikika akitoa kauli kama “Mapinduzi Daima” “Udumu Muungano” “Kidumu Chama cha Mapinduzi” n.k.

Maalim Seif alipoanza kushika madaraka ya Uwaziri Kiongozi alionekana kuwa ni mtetezi wa Umma na Mwana Mapinduzi madhubuti asiyeyumba, muumini wa kweli wa Muungano na kiongozi safi wa CCM. Kumbe alikuwa mnafiki alikuwa chui aliyevaa ngozi ya Kondoo, alikuwa akicheza watu shere. Lengo lake katika kuyafanya yote hayo lilikuwa ni kujitafutia umaarufu tu, ili apate kuaminiwa na hatimae akikabidhiwa madaraka aweze kutekeleza lengo lake.

Kwa maelezo yake mwenyewe Maalim Seif, anadai kuwa yeye na kundi lake walikuwa wakiendesha siasa za Upinzani dhidi ya SMZ wakiwa kwenye Serikali na Chama cha Mapinduzi. Ndipo ilipogunduliwa njama ya Seif Shariff na kundi lake la kukihujumu Chama cha Mapinduzi, suala hili liliwasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa na baada ya mjadala mrefu na kuthibitika kuwa Seif na wenzake wamekiuka miiko ya uwanachama na uongozi wa CCM, ndipo Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ilipoamua kuwafukuza Uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi Seif Shariff na wenzake wengine saba. Ambao ni Seif Sharif Hamad, Shaaban Khamis Mloo, Hamad Rashid Mohammed, Ali Haji Pandu, Masoud Omar, Soud Yussuf Mgeni, Rashid Hamadi Hamadi na Khatib Hassan Khatib

Pamoja na kuwa Chama cha Mapinduzi kimechukua hatua za kuwafukuza Uwanachama watu hao baada ya kupata uthibitisho kuwa kutokana na matendo yao hawawezi tena kuendelea kuwa Wanachama wa CCM. Lakini kundi la watu hao walipofika Zanzibar walidai kuwa awameonewa. Na Chama cha Mapinduzi katika kufikia uamuzi wake wa kuwafukuza Uwanachama awatu hao, haki haikutendeka, na kwa upande wao wahusika walikuja Zanzibar na kupita sehemu mbali mbali huku wakidai kuwa wameonewa.Tofauti na kauli aliyotoa mwenyewe Maali Seif katika moja ya hotuba yake akihutubia wanachama wa Chama chake kuwa Chama chao cha CUF kina mizizi mirefu kwani harakati zake zilianza tangu iaka ya 80 wakati wa Utawala wa Mzee Aboud Jumbe kama tunakumbuka wakati huo walianza na P.L.O (Pemba Liberation Organization), huku wenyewe wanajisifu kuwa ilifanya kazi kubwa ya kumuondoa madarakani Rais Abouid Jumbe mnamo mwaka 1984. Katika kuthibitisha kwao kuwa walikuwa wapinzani ndani ya CCM na Serikali zake wasaliti hawa mnamo mwaka wa 1988 – 1992
Walianzisha harakati za upinzani wa chini kwa chini kwanza walianza kwa kuanzisha kikundi cha “BISMILAHI’, na baadae kubadilika na kua “HAMAK”, baada ya muda mdogo tu wakabadilisha na kuwa “KAMAHURU” ambayo iliongozwa na Mwenyekiti Shaaban Khamis Mloo; Katibu Mkuu wake alikuwa Ali Haji Pandu na wajumbe wengine
walikuwa ni Soud Yussuf Mgeni, Suleiman Seif Hamad na baadhi ya wafuasi wa Maalim Seif ambao ameanza nao harakati hizi. Kikundi hiki cha upinzani kilichoongozwa na Maalim Seif kilikuwa na lengo la kupinga Uongozi wa Chamamcha Mapinduzi, Serikalia ya Mapainduzi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ilipoingia miaka ya 1990 kilijigeuza jina na kuwa ZUF, (Zanzibar United Front). Kwa kuwa upinzani kwa kipindi hicho ndani ya Tanzania ulikuwa bado haujaruhusiwa kisheria, ndipo Serikali za CCM ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilichukua hatua za kuudhibiti uchochezi huo kwa kuchukuwa hatua kadhaa za kisheria, Vyombo vya dola wakati vinachukua hatua za kuwashughulikia wale wote waliodhaniwa kuwa wanavunja sheria ndipo Maalim Seif kaatika kusachiwa nyumbani kwake alikutwa na nyaraka za Serikali, nyaraka ambazo hakutakiwa kuwa nazo kwa mujibu wa Sheria kwani nyaraka hizo zilikuwa ni za siri za Serikali wakati yeye sio Kiongozi tena wa Serikali. Kutokana na kadhia hiyo Seif Shariff ilibidi kufunguliwa mashitaka kutokana na kosa la kukutwa na nyaraka za siri za Serikali.

Pamoja na kufunguliwa mashitaka Mahakamani. Baada ya Maalaim Seif kufikishwa Mahakamani na kusomewa shitaka lake, Serikali ilibidi kuendelea na uchunguzi na ili mshtakiwa asije akapoteza ushahidi Mahakama iliamua kumnyima dhamana mshitakiwa na kuwekwa rumande kwa muda usiopungua miaka 30 sawa na mwaka mmoja na nusu.

Wakati Seif Sharif akiwa Mahabusu huku nyuma wafuasi wake waliendeleza uhasidi na ufisadi dhidi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Waliendelea kutumia mali za Serikali na kwa Pemba waliendesha Kampeni kuhakikisha kila mzaliwa wa Pemba lazima akubaliane na matakwa yao. Mbinu walizozitumia katika kuwafanya watu wa Pemba wakubaliane nao ni kuzua uongo kuwa kiongozi wao amewekwa kizuizini na kubambikizwa kesi isiyokuwa ya kweli, watu wa Pemba wanaonewa na watu wa Unguja na Zanzibar inamezwa na Tanzania Bara. Kwa hivyo walianzisha kampeni za kuwachochea wananchi kudai kura ya maoni juu ya muundao wa Muungano, eti kwa sababu wakati ulipoanzishwa. Suala la kura ya maoni lilikuwa ndio sera yao, wachochezi hawa wa chini kwa chini waliliremba na kulipaka mafuta na hatimae likawa linazungumzwa kwenye vikundi vyao kila wanapokutana. Wachochezi hawa kwa kuwa walikuwa wanataka kuyateka mawazo ya watu wa Zanzibar ilibidi kuwambia uongo kuwa Muungano unaikandamiza Zanzibar na kwa kuwa Zanzibar ilikuwa inakabiliwa na hali ngumu ya Kiuchumi kutokana na kushuka bei ya zao la karafuu, zao ambalo lilikuwa ndio zao pekee lililotegemewa kwa uchumi wa Zanzibar. Basi suala la hali ngumu ya uchumi wa Zanzibar moja kwa moja likanasabishwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa hivyo wachochezi hawa wakaanza kazi ya kuwachochea Wapemba kwa kuwaambia kuwa wanaonewa na Waunguja. Na wanapokuwa Unguja waliwaambia watu wa Unguja kuwa Tanzania Bara imeimeza Zanzibar kupitia Muungano na hali ndio maana imekuwa ngumu katika uchumi na maendeleo ya jamii. Wachochezi hawa wanapokuwa Tanzania Bara walikuwa wanawaambia Watanzania wenye imani ya dini ya Kiislamu kuwa Uislamu unapigwa vita na Serikali, walikuwa wanatoa vigezo kama cha Waislamu kuwa nyuma ki-elimu, kuwa na idadi ndogo ya viongozi wenye imani ya kiislamu katika Wizara za Serikali na vyombo vya Dola, jambo ambalo lilipelekea kujitikeza baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kuwa na misimamo mikali ya kidini na kuanza kupambana na vyombo vya Dola. Mfano uliyo hai ni matukio mawili ya vurugu zilizoanzishwa na wafuasi hao kuhusiana na Dini, moja ni lile la maandamano ya kidini yaliyofanywa hapa Zanzibar kwa kudaiwa kupinga kauli ya kiongozi mmoja wa UWT kudai wanawake waolewe na mume zaidi ya mmoja. Maandamano mengine ni yale yaliyofanyika mjini Dar es Salaam katika Mtaa wa Magomeni Mwembechai yanayodaiwa yamefanyika kupinga kuuzwa nyama za Nguruwe katika Mabucha.

Maandamano yote hayo yaliyofanyika Zanzibar na Dar es Salaam yalikuwa hayana mnasaba na Dini bali lengo lilikuwa ni kuendesha upinzani dhidi ya Chama cha mapinduzi na Serikali zake. Sababu kubwa iliyopelekea maandamano hayo kuonekana kuwa si maandamano ya kidini ni kuwa, waandamanaji waliamua kupiga askari wa vyombo vya Ulinzi wa nchi yetu, kuvamia Afisi za Chama cha Mapinduzi na kuharibu mali za Serikali kama magari Afisi na kadhalika. Katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali wa mwaka l990, Maalim Seif na kundi lake walielekeza nguvu zao Pemba kwa kufanya kampeni ya kuwazuwia wananchi wasijiandikishe kuwa wapiga kura. Na kama inavyoeleweka kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi mwananchi kma hakujiandikisha kuwa mpiga kura basi anakuwa amepoteza haki yake ya kupiga kura. Kama kawaida yao, walipoona kampeni yao haiungwi mkono na wananchi wengi walianzisha mtindo wa kutumia vitisho dhidi ya wale wote walioonyesha kukaidi amri yao ya kutokwenda kujiandikisha. Wananchi walitishwa kwa kuambiwa akuwa atakaekwenda kujiandikisha basi adabu yake ni kugomewa. Wale walioonekana kuwa na msimamo tofauti waliviziwa njiani walipokuwa wanatoka katika vituo vya kujiandikisha na kunyang’anywa Kadi zao za kujiandikisha. Kwa wale wananchi walioamua kutumia haki yao ya kujiandikisha, iliwalazimu kujiandikisha kwa njia za kificho ili wasijulikane kuwa wamejiandikisha, iliwalazimu kujiandikisha kwa njia za kificho ili wasijulikane kuwa wamejiandikisha. Na wale wote waliobainika kuwa wamejiandikisha walisusiwa,walipakiwa kinyesi nyumba zao, wengine nyumba zao zilitiwa moto, waling’olewa mazao yao mashambani, mashamba yao ya Mikarafuu yalitiwa moto, wanawake waliachwa na waume zao na wanaume wameachishwa na wake zao. Wachochezi hao walidiriki hata kuvihujumu vituo vya kujiandikisha wapiga kura kwa kuvipaka kinyesi cha binadamu na hata kuvichoma moto. Matukio haya yalisababisha uandikishaji wa wapiga kuraa katika Uchaguzi Mkuu wa 1990 kwa upande wa Pemba kutokufanikiwa vizuri, kwani wananchi wengi hawakuweza kujiandikisha. Waliojiandikisha wengi wao ni wale wananchi waliojitolea muhanga pamoja na wengi wa Watumishi wa Serikali tu.

Matukio haya ya upinzani wa chini kwa chini na kubakia na baadhi ya viongozi bdabi ya Chama na Serikali ambao wanashirikiana na wapinzani katika kupinga na kuleta hujuma kwa Serikali, huenda ikiwa ni miongoni mwa sababu iliyopelekea Chama cha Mapinduzi kuamua kuanzisha mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini ili kuondoa shari licha ya mfumo huo kupingwa na wananchi walio wengi kama ilivyoelezwa na Tume ya Nyalali. Dhana ilikuwa ni kwamba ukianzishwa mfumo huu wapinzani hao hawatokuwa na sababu tena ya kuendesha siasa za uhasama na kwamba utajitokeza utamaduni wa kupingana bila kupigana, kutofautiana bila kugombana. Lakini lililojitokeza kwa wapinzani hao ni kinyume kabisa na lengo lililokusudiwa. Kutokana na kuonekana kuwa wana ajenda yas siri ambayo haiwafikiani na taraatibu za kidemokrasia. Ndipo CCM ilipoamua kwa makusudi kuanzisha Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini. Kwa kipimo chochote kile, Tanzania imejitahidi mwisho wa kikomo chake kuingiza nchini Mfumo wa Vyama vingi. Na ikatoa nafasi kwa vyama mbali mbali kujitokeza na kuchangia katika utaratibu huu na wakati huo huo ikafaulu kudumisha amani na mshikamano wa Kitaifa. Imefikia mahali ambapo Tanzania iliwaachilia wananchi waamue wenyewe juu ya mustakabali wao wa kisiasa.

Baada ya kukubaliwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, na kutolewa masharti ya aina ya vyama vinavyokubalika. Kikundi kilichokuwka cha uchochezi cha ZUF (Zanzibar United Front) kilichokuwa kikionbgozwa na Bwana Shaaban Khamis Mloo akiwa Mwenyekiti wa Bwana Ali Haji Pandu Katibu Mkuu wake, waliungana na Chama cha Wananchi cha Bwana James Mapalala na kuunda chama akilichoitwa Civic United Fron (CUF) ili kupata Chama cha Kitaifa. Kabla kikundi hiki cha ZUF kilikuwa na lengo la kujigeuza kuwa Chama cha Siasa bila ya kuungana na kikundi chochote kutoka Tanzania Bara. Kwani kikundi hiki hakikuwa na haja ya kupata wafuasi kutoka Tanzania Bara, kwani lengo lake lilikuwa ni Zanzibar pekee. Kujiunga kwake na kikundi cha Bwana James Mapalala ilikuwa ni mkakati tu, wa kupata Usajili wa Chama chao.

Baada tu, ya kupata usajili Chama cha CUF, wafuasi wake wakacharuka kuweka bendera kila pahali jambo ambalo lilikuwa ni kinyume cha Sheria na taratibu za nchi. Maalim Seif akiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, alianza kupeperusha bendera kwenye gari yake na kujifanya kuwa sawasawa na Rais wa nchi.