Monday, July 9, 2007

JKAMPENI ZA UCHAGUZI MWEZI WA RAMADHANI

Ndugu Mhariri,

Napenda kuomba nafasi kupitia gazeti lako kutoa maoni yangu kuhusiana na mwenendo wa Uchaguzi unaoenedelea hivi sasa nchini tukiwa kwenye kipindi cha Kampeni.

Kwanza sina budi kutoa pongezi zangu kwa Chama Cha Mapinduzi kwa utaratibu wake wa kufanya mikutano ya Kampeni wakati wa asubuhi ili wanachama wake wapate nafasi ya kujitafutia riziki na kufanya Ibada katika kipindi hichi cha Ramadhani sote ni welewa wa mambo kuwa fadhila za mwezi wa Ramadhani kwa wanaofanya Ibada ni kubwa sana kuliko miezi mengine yoyote ya Kiislamu. Aidha Waisalamu wanatakiwa wawe waaminifu, wakweli na waungwana na kuepukana na kauli ambazo zitawafanya wasitafautiane na wale wasiofunga katika kipindi hichi. Vile vile yale yaliyomo kwenye dhamira zao yafuatane na vitendo vyao.

Nimeamua kutumia neno dhamira kwa kuwa ndio inayomuhukumu mtu hata kama jambo hajalifanya ila anakusudia kulifanya kwani tunaambiwa kwenye hadithi za Mtume kuwa “Hakika vitendo vinafuatana na nia na kila mtu atalipwa kutokana na nia yake” Kutokana na kukaribia Uchaguzi Mkuu na huku baadhi ya vyama tayari vishakata tamaa ya ushindi licha ya kutamka kuwa vitashinda hadharani ili kuwapa moyo wafuasi wake na kuwalaghai kwa ajili ya lengo lao waliloliweka na hasa baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 30/10/2005. Nimeamua kusema kuwa baadhi ya vyama vya Siasa vimekata tama ni kutokana na ushahidi nilionao wa watu hao kutumia mikutano ya siri na kututaka tujitayarishe kwa maandamano makubwa baada ya Uchaguzi ya kudai kupokonywa ushindi kinachonishangaza na kinachonifanya kuamua kuandika barua hii ni kutaka kuwatahadharisha wananchi wenzangu kuwa suala la kunyanganywa ushindi kwa atakaeshinda halitowezekana hata kidogo kutokana na taratibu nzuri zilizoandaliwa za kuhesabu kura na kutangaza matokeo kwa jumla ambapo vyama vyote vinatakiwa kuweka Mawakala bila ya shaka sote ni mashuhuda wa kauli za viongozi wakuu wote wa Vyama na hasa Chama Cha CUF ambao wamekiri wenyewe kuwa utaratibu ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi utapelekea kufanyika kwa Uchaguzi huru na wa haki. Sasa kinachonishangaza na kunifanya nikumbuke swaltul-Munafiqina ambayo imewaeleza kwa urefu na mapana watu ambao dhamira zao siku zote haziendeda na kauli zao ni kutaka kujua hayo maandamano wanayotaka kufanya ni kwa ajili ya nini na maslahi ya nani ikiwa tayari tumejenga uaminifu kwa Tume na tumekubali kuyapokea matokeo ya kura na haya ya Urais. Hivi viongozi wa CUF wanapotutaka siku watakayotutangazia kwa siri maandamano waliyoyatayarisha na kututaka tushiriki na kuwatanguliza wazee mbele kwa kile wanachokidai kuwa wakifa wao si hasara kwa kuwa washaonja chumvi nyingi na baadae wafuatie vijana na mwisho wanawake. Hivi ni kweli hawa viongzoi wa CUF wanaitakiwa mema nchi yetu na sisi wananchi?.

Jambo ninalotaka kuwaambia viongozi wa CUF ni kuwa wananchi wengi hivi sasa si wajinga na wanathamini uhai wao na wanafahamu kuwa mfa maji hukamata maji, kwa hiyo wasiwe na tamaa ya kutufanya chambo kwa kuwa tu bwana mmoja kakosa Urais. Hayo maandamano yake atakayoyafanya atayafanya yeye na Bwana Said wake ambao wamekula kiapo cha kufa kwa ajili yake na wale waliokata tamaa ya maisha lakini wengi tumechoka na ule wimbo wetu wa akikosa Seif tumekosa sote. Tukumbuke kuwa kupata au kukosa yote ni Majaaliwa. Na Mola amesema kuwa humpa Ufalme amtakae na humnyima amtakae. Hivi Maalim Seif akikosa yeye ndio atake sisi atufanye kuku wa muhanga? Kwa hilo tunamwambia hawai na tunamtakia kila la kheri katika maandamano atakayoyaongoza na kuzungukwa na hao wakubwa wake. Mwisho nawataka viongozi wa CUF wasome Shishtul Munafinna na hasa aya ya nane ya sura hiyo mwisho kabisa nawataka wana CUF wajue kuwa akishindwa Seif safari hii tisichoke kwani 2010 haiko mbali panapo uhai tumpe tena nafasi kwani kuvunjika kwa koko sio mwisho wa utunzi. La muhimu kwetu ni “AMANI” kwani hiyo ndio siri ya mafanikio na maendeleo na sio “UPANGA” utakaotupeleka kwenye hilaki. Mola tunakuomba utudumishie AMANI yetu dhidi ya Mahasidi wa nchi yetu. AMIN


RAIA MWEMA
ZANZIBAR

No comments: