Monday, July 9, 2007

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama na wafuasi wake kutobabaika na kauli zilizotolewa na CUF za kudai kwamba kuna vijana wengi wa CCM wamejiunga na chama hicho cha upinzani.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Bwana Vuai Ali Vuai, +imeeleza kuwa kauli hizo ni za uongo na hakuna mwanachama yeyote aliyehama CCM na kujiunga CUF.

Bwana Vuai ameeleza kuwa baada ya kufuatilia kauli hiyo katika maeneo yaliyoelezwa kwamba kuna vijana waliojiunga na chama hicho, CCM imebaini kuwa taarifa hizo zilikuwa hazina ukweli.

Ameeleza kwamba kutokana na kufuatilia huko imefahamika vijana waliotangazwa kutoka CCM ni miongoni mwa vijana wa chama hicho cha upinzani wa maeneo ya Shangani huko Mkokotoni ambao walipangwa kurejesha kadi za kughushi ambazo hazikuwa kadi halali za CCM.

Amewataka wananchi kutobabaishwa na propaganda za uongo ambazo ni mfululizo wa kauli za upotoshwaji zinazotolewa na viongozi wa CUF kwa vipindi chote hata kabla ya kuanza kwa mikutano ya kampeni.

Bwana Vuai alisema viongozi wa upinzani wamekuwa wakifanya hivyo kwa kufahamu kwamba CCM itaendelea kushinda katika uchaguzi ujao Tanzania Bara na Zanzibar kutokana na kukubalika kwake mbele ya jamii.

Alifahamisha kuwa ushahidi wa CCM kuendelea kuongoza nchi unabainika kutokana na chama hicho kushinda viti 200 kabla ya hata uchaguzi vikiwemo viti vinane (8) vya ubunge na 192 udiwani.

Alieleza kuwa hicho ni kigezo tosha cha kuthibitisha kwamba wananchi wameridhika na utekelezaji wa ilani za CCM za mwaka 2000 ilisababisha kuimarika kwa miundo mbinu ya kiuchumi na ustawi wa jamii nchini.

Hivyo, Bwana Vuai ameitaka CUF kuacha mara moja kutoa kauli za kubabaisha kwani kufanya hivyo ni kuzidi kuidhihirishia dunia kuwa tayari kimekata tamaa ya kupata ushindi kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 30, mwaka huu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI


………………
(Vuai Ali Vuai)
Katibu – Idara ya Itikadi na Uenezi
Chama cha Mapinduzi
ZANZIBAR

20/10/2005

No comments: